399 Njia ya Kumwaamini Mungu Ndiyo Njia ya Kumpenda

1 Njia ya kuamini katika Mungu ni njia ya kumpenda Yeye. Ikiwa unaamini katika Yeye lazima umpende Yeye; kwa hali yoyote, kumpenda Yeye hakuhusu tu kulipa upendo Wake au kumpenda kwa kutegemea hisia za dhamiri—ni pendo safi kwa Mungu. Ukitumia tu dhamiri yako hutaweza kuamsha upendo wako kwa Mungu; unapohisi kweli kupendeza Kwake ndani ya moyo wako roho yako itasisimuliwa na Yeye, na ni wakati huo tu ndio dhamiri yako itaweza kufanya kazi yake ya asili. Hiyo ni kusema kwamba watu wakishasisimuliwa na Mungu katika roho zao na wakati roho zao zimepata maarifa na himizo, yaani, baada ya wao kupata uzoefu, ndipo tu wataweza kumpenda Mungu kwa kufaa na dhamiri zao.

2 Kumpenda Mungu na dhamiri yako si vibaya—hiki ni kiwango cha chini sana cha kumpenda Mungu. Njia ya wanadamu ya upendo ya kufanya haki kwa shida tu kwa neema ya Mungu bila shaka haiwezi kuchochea kuingia kwao kiutendaji. Watu wanapopata baadhi ya kazi ya Roho Mtakatifu, yaani, wanapoona na kuonja upendo wa Mungu katika uzoefu wao wa vitendo, wakiwa na maarifa fulani ya Mungu na kuona kweli kwamba Mungu anastahili sana upendo wa wanadamu na jinsi Alivyo mzuri, ni wakati huo tu ndio watu wanaweza kumpenda Mungu kwa uhalisi.

3 Upendo halisi kwa Mungu hutoka ndani ya kina cha moyo; ni upendo uliopo tu kwa msingi wa wanadamu kumfahamu Mungu. Watu wasipokuwa na ufahamu wa Mungu wanaweza tu kumpenda Yeye kulingana na upendeleo wao wenyewe na fikira zao binafsi; aina hiyo ya upendo haiwezi kuitwa upendo wa hiari, wala haiwezi kuitwa upendo halisi. Mara tu mtu anapokuwa na ufahamu wa Yeye, inaonyesha kwamba moyo wake umemrudia Mungu kwa ukamilifu, inaonyesha kwamba upendo wake halisi kwa Mungu ndani ya moyo wake ni wa hiari. Mtu wa aina hiyo pekee ndiye ana Mungu ndani ya moyo wake.

Umetoholewa kutoka katika “Upendo Halisi kwa Mungu ni wa Hiari” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 398 Unapaswa Kutafuta Kumpenda Mungu Katika Imani Yako

Inayofuata: 400 Ufuatiliaji Unaopaswa Kufuatwa na Waumini

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp