601 Njia za Petro na Paulo

1 Je, nyote mnaishika njia gani sasa? Ikiwa hamjafikia ufuatiliaji wa maisha, wa kujifahamu, au kumfahamu Mungu kama Petro, basi hiyo bado si njia ya Petro. Hivi sasa watu wengi wako katika aina hii ya hali: “Ili kupata baraka ni lazima nijitumie kwa ajili ya Mungu na kulipa gharama kwa ajili Yake. Ili kupata baraka ni lazima niache kila kitu kwa ajili ya Mungu; lazima nikamilishe kile ambacho ameniaminia na kutekeleza wajibu wangu vizuri.” Hili linatawaliwa na nia ya kubarikiwa; ni kutumika kwa kusudi la kupata thawabu za Mungu, kwa ajili ya kupata taji. mtu wa aina hii hana ukweli ndani ya moyo wake, na hakika anaelewa tu maneno fulani ya mafundisho ya dini ambayo anaringia kila mahali. Njia yake ni njia ya Paulo.

2 Ingawa huwezi kupanga kuishika njia ya Paulo, asili yako inakutawala kwa njia hii, na unaelekea upande huo bila kupenda. Ingawa unataka kuishika njia ya Petro, ikiwa hufahamu vizuri jinsi ya kulifanya hilo, basi bado utaishika njia ya Paulo bila kupenda—huu ni ukweli wa hali hiyo. Inaweza kusemekana kwamba Mungu amewafichulia sasa njia ya kuokolewa naye na ya kukamilishwa. Hii ni neema ya Mungu na kutia moyo na ni Yeye anayewaongoza kwenye njia ya Petro. Bila uongozi na kupata nuru kutoka kwa Mungu hakuna ambaye angeweza kuishika njia ya Petro; chaguo la pekee lingekuwa kuelekea kwa njia ya Paulo, kuzifuata nyayo za Paulo kuelekea kwa uharibifu.

3 Njia ya Paulo haikuhusisha kujijua au ufuatiliaji wa mabadiliko katika tabia. Hakuchangua kamwe asili yake mwenyewe na hakuwa na ufahamu wa kile alichokuwa; alijua tu kwamba alikuwa mkosaji mkuu katika kumtesa Yesu. Hakuwa amepata ufahamu hata kidogo wa asili yake mwenyewe, na baada ya kumaliza kazi yake alihisi kwamba alikuwa Kristo na anapaswa kupewa thawabu. Kazi ambayo Paulo alifanya ilikuwa tu kutoa huduma kwa Mungu. Kwake mwenyewe, ingawa alipokea ufunuo kiasi kutoka kwa Roho Mtakatifu, hakuwa na ukweli au uzima hata hivyo. Hakuokolewa na Mungu—aliadhibiwa.

4 Kwa nini inasemekana kwamba njia ya Petro ni njia ya kukamilishwa? Kwa sababu katika utendaji wake alizingatia hasa uzima, alifuatilia ufahamu wa Mungu, na akazingatia kujifahamu. Kupitia uzoefu wake wa kazi ya Mungu alikuja kujijua, alipata ufahamu wa hali potovu za mwanadamu, alijua kasoro zake, na ni jambo gani lilikuwa muhimu sana kwa mwanadamu kulifuatilia. Aliweza kumpenda Mungu kwa dhati, alijua jinsi ya kumlipa Mungu, alipata ukweli kiasi, na alikuwa na ukweli ambao Mungu huhitaji. Kutoka kwa vitu vyote alivyosema wakati wa majaribio yake, inaweza kuonekana kwamba Petro alikuwa kweli mwenye ufahamu zaidi wa Mungu. Kwa sababu alielewa ukweli mwingi sana kutoka kwa maneno ya Mungu, njia yake ikawa yenye kung’aa zaidi na zaidi na kuzidi kufungamana na mapenzi ya Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kuitembea Njia ya Petro” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 600 Kufanikiwa ama Kushindwa Kunategemea Njia Atembeayo Mwanadamu

Inayofuata: 602 Njia ya Imani ya Mafanikio Katika Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp