528 Watu Hawatendi Kabisa Maneno ya Mungu

1 Mungu hana maneno zaidi ya kunena, lakini watu hawajaenda kwa kasi sawa kabisa, na wamebaki nyuma kabisa, hawawezi kukaa karibu na kila hatua, hawawezi kuzifuata nyayo za Mwanakondoo kwa karibu. Kile ambacho walipaswa kukitii hawajakitii; kile ambacho walipaswa kukitenda hawajakitenda; kile ambacho walipaswa kukiomba hawajakiomba; kile ambacho walipaswa kukiacha hawajakiacha. Bado hawajafanya kitu chochote kati ya hivi. Kwa hiyo, mazungumzo haya ya kuhudhuria karamu ni maneno matupu; hayana maana yoyote halisi na yote yamo katika fikira zao. Ikitazamwa kutoka leo, inaweza kusemwa kwamba hadi sasa watu hawajatimiza wajibu wao hata kidogo. Kila kitu kinategemea Mungu kufanya na kusema vitu Yeye Mwenyewe. Kazi ya mwanadamu kwa kweli imekuwa ndogo sana; watu ni taka isiyokuwa na maana ambao hawana uwezo wa kushirikiana na Mungu.

2 Mungu amenena mamia ya maelfu ya maneno, lakini watu hawajayaweka katika vitendo kabisa—iwe ni kuukana mwili, kuacha dhana, kuwa watiifu kwa Mungu katika mambo yote huku ukikukuza ufahamu na kupata umaizi, kutowapa watu nafasi mioyoni mwao, kuondoa sanamu ambazo zinamiliki mioyo yao, kuasi dhidi ya makusudi yao binafsi ambayo si sahihi, kutotenda kwa msingi wa mihemko yao, kufanya mambo kwa haki na bila ubaguzi, kuyafikiria zaidi masilahi ya Mungu na ushawishi wao kwa wengine wanapozungumza, kufanya mambo zaidi yanayonufaisha kazi ya Mungu, kufikiri kuhusu kuinufaisha nyumba ya Mungu katika yote wanayofanya, kutoruhusu mihemko yao ziiamuru tabia yao, kuacha yale ambayo yanapendeza miili yao wenyewe, kuondoa maoni ya zamani ya ubinafsi, na kadhalika. Lakini watu hawajayaweka katika vitendo kabisa.

3 Kwa kweli watu wanafahamu baadhi ya mahitaji haya ambayo Mungu anahitaji kutoka kwa mwanadamu, lakini hawako tayari kuyaweka katika vitendo. Ni kwa namna gani nyingine ambayo Mungu anaweza kufanya kazi na kuwashawishi? Waasi machoni pa Mungu wanawezaje bado kuwa na ujasiri wa kuchukua maneno Yake na kuyastahi? Wanawezaje kuwa na ujasiri wa kula chakula cha Mungu? Dhamiri ya watu ipo wapi? Hawajatimiza wajibu mdogo kabisa waliopaswa kutimiza, sembuse kufanya yote wawezayo. Je, wao si watu wa njozi tu? Hakuwezi kuwa na mazungumzo ya uhalisi bila matendo. Huo ni ukweli wa wazi!

Umetoholewa kutoka katika “Sisitiza Uhalisi Zaidi” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 527 Maana ya Kweli ya Maneno ya Mungu Haijawahi Kueleweka

Inayofuata: 529 Usijifurahishe kwa Sababu Mungu ni Mvumilivu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp