571 Watu Hawamtendei Mungu kama Mungu

1 Kila mtu kila wakati, na mara nyingi hufanya hesabu kama hizi ndani ya mioyo yao, na wao wanatoa madai yao kwa Mungu yanayoonyesha motisha yao na malengo na mipango. Hivi ni kusema, ndani ya moyo wake binadamu siku zote anamweka Mungu majaribuni, siku zote anaunda njama kumhusu Mungu, na kila wakati anabishana na Mungu kuhusu kesi yake na kujaribu kumfanya Mungu kutoa kauli, ili aweze kuona kama Mungu anaweza kumpa kile anachotaka au hawezi. Wakati huohuo akimfuata Mungu, binadamu hamchukulii mungu kama Mungu. Siku zote amejaribu kufanya mipango na Mungu, akitoa madai bila kusita kwake Yeye na hata akimsukuma Yeye kwa kila hatua, akijaribu kupiga hatua ya maili licha ya kupewa inchi moja.

2 Wakati huohuo akijaribu kuunda mipango na Mungu, binadamu pia anabishana na Yeye, na wapo hata watu ambao, wakati majaribio yanapowapata au wanapojipata katika hali ya kuteketea, mara nyingi wanakuwa wanyonge, wananyamaza na kuzembea katika kazi yao, na wanajaa malalamiko kuhusu Mungu. Tangu wakati ule alipoanza kusadiki Mungu, binadamu amemchukulia Mungu kama alama ya pembe inayoonyesha wingi wa neema, kisu cha Kijeshi cha Uswisi, na amejichukulia yeye mwenyewe kuwa mdaiwa mkubwa zaidi wa Mungu, ni kana kwamba kujaribu kupata baraka na ahadi kutoka kwa Mungu ni haki yake ya asili na jukumu, huku jukumu la Mungu likiwa ni kulinda na kutunza binadamu na kumtosheleza. Huu ndio uelewa wa kimsingi wa “imani katika Mungu” wa wale wote wanaosadiki Mungu, na uelewa wao wa kina zaidi wa dhana ya imani katika Mungu.

3 Kutoka kwenye kiini cha asili ya binadamu hadi katika ufuatiliaji wake wa kibinafsi, hakuna kitu chochote kinachohusiana na kumcha Mungu. Nia ya binadamu kwa kusadiki Mungu huenda isiwe na uhusiano na kuabudu Mungu. Hivi ni kusema kwamba, binadamu hajawahi kufikiria wala kuelewa kwamba imani katika Mungu inahitaji kumcha Mungu, na kumwabudu Mungu. Ni kwamba moyo wa binadamu una kijicho, unabeba udanganyifu na ujanja, haupendi mambo ya kutopendelea na haki, au kile kilicho kizuri, nao ni wenye kuleta dharau na ulafi. Moyo wa binadamu usingeweza kumzuia Mungu zaidi, hajaupatia Mungu kamwe. Mungu hajawahi kuona moyo wa kweli wa binadamu, wala hajawahi kuabudiwa na binadamu.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 570 Mwanadamu Hana Imani ya Kweli Katika Kristo

Inayofuata: 572 Hii ni Imani ya Kweli Katika Mungu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

83 Upendo wa Kweli

1 Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao, nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini. Neno Lake linanijaza na raha na furaha...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki