409 Watu Hawamwamini Mungu kwa Kweli

1 Katika miaka mingi ya kazi Yangu, mwanadamu amepokea vitu vingi na kujinyima vitu vingi, lakini bado Nasema kuwa mwanadamu haniamini kikamilifu. Kwa maana mwanadamu anakubali kijuujuu tu kuwa Mimi ni Mungu lakini hakubaliani na ukweli Ninaounena, sembuse kuuweka ukweli katika matendo Ninavyohitaji kwake. Hiyo ni kusema, mwanadamu anakubali tu uwepo wa Mungu, lakini sio ule wa ukweli; mwanadamu hukubali tu uwepo wa Mungu, lakini sio wa uzima; mwanadamu anakubali tu jina la Mungu, lakini sio kiini Chake. Kutokana na ari yake, mwanadamu amekuwa chukizo mbele Zangu. Kwa kuwa mwanadamu anatumia tu maneno yanayofurahisha masikio kunihadaa, na hakuna anayeniabudu kwa moyo wa kweli.

2 Maneno yenu yanabeba majaribu ya ibilisi. Na maneno yenu ni yenye kiburi kupindukia, ni vile tu kama yamesemwa na malaika mkuu. Zaidi ya hayo, matendo yenu yamechakaa; tamaa zenu zisizo na kiasi na nia zenu zenye tamaa ni za kukera zikisikizwa. Nyote mmegeuka nondo katika nyumba Yangu, vyombo vya kukataliwa na chukizo. Kwa maana hapana kati yenu ambao ni wapenda ukweli, bali ni wanadamu wanaopenda baraka tu, walio na matamanio ya kupaa mbinguni, na ya kumwona Kristo anapoonyesha nguvu Zake duniani. Lakini mmewahi kuwaza jinsi mwanadamu kama ninyi, aliyepotoka sana, na asiyejua kabisa Mungu ni nini, angestahili kumfuata Mungu? Mnawezaje kupaa mbinguni? Mnawezaje kustahili kuuona uzuri wa ukuu usio na kifani?

Umetoholewa kutoka katika “Wengi Wanaitwa, Lakini Wachache Wanachaguliwa” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 408 Kweli Umeyatoa Maisha Yako Katika Imani Yako?

Inayofuata: 410 Bado Una Imani Iliyokanganywa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp