509 Watu Wanaopatwa na Mungu Wamemiliki Uhalisi

1 Mungu ni Mungu wa uhalisi: kazi Zake zote ni halisi, maneno yote Anayoyanena ni halisi, na ukweli wote Anaouonyesha ni halisi. Kila kisicho maneno Yake ni kitupu, kisichokuwepo, na kisicho timamu. Leo, Roho Mtakatifu yupo kwa ajili ya kuwaongoza watu katika maneno ya Mungu. Ikiwa watu wanatafuta kuingia katika uhalisi, basi ni lazima wauandame uhalisi, na waujue uhalisi, baadaye ni lazima wapitie uhalisi, na kuishi kwa kudhihirisha uhalisi.

2 Kadiri watu wanavyoujua uhalisi zaidi, kadiri wanavyoweza kugundua ikiwa maneno ya wengine ni halisi; kadiri watu wanavyojua uhalisi zaidi, ndivyo wanavyokuwa na dhana chache zaidi; kadiri watu wanavyopitia uhalisi zaidi, kadiri wanavyojua zaidi matendo ya Mungu wa uhalisi, na ndivyo inavyokuwa rahisi kwao kujiweka huru kutokana na tabia zao potovu na za kishetani; kadiri watu walivyo na uhalisi mkubwa, ndivyo wanavyomjua Mungu zaidi na kuuchukia mwili zaidi na kupenda ukweli; na kadiri watu walivyo na uhalisi mkubwa, ndivyo wanavyofika karibu na ubora wa mahitaji ya Mungu.

3 Watu waliopatikana na Mungu ni wale walio na uhalisi, na wanaojua uhalisi; wale ambao wamepatikana na Mungu wamepata kuyajua matendo halisi ya Mungu kutokana na kupitia katika uhalisi. Kadiri hasa unavyoshirikiana zaidi na Mungu na kuudhibiti mwili wako, ndivyo utakavyopokea zaidi kazi ya Roho Mtakatifu, ndivyo utakavyopata uhalisi zaidi, na ndivyo utapatiwa nuru zaidi na Mungu—na hivyo ukubwa wa ufahamu wako wa matendo halisi ya Mungu. Ikiwa unaweza kuishi katika mwangaza wa sasa wa Roho Mtakatifu, njia ya sasa ya kutenda itakuwa wazi kwako, na utaweza kujitenga zaidi na dhana za kidini na vitendo vilivyopita zamani. Leo tunalenga uhalisi: Kadiri watu walivyo na uhalisi zaidi, ndivyo ufahamu wao wa ukweli unavyokuwa wazi, na ufahamu wao wa mapenzi ya Mungu unaongezeka.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kujua Uhalisi” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 508 Lenga Kutenda Ukweli Ili Ukamilishwe

Inayofuata: 510 Lazima Umshuhudie Mungu Katika Vitu Vyote

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp