87 Mungu Mwenye Mwili wa Siku za Mwisho Humkamilisha Mungu kwa Maneno

1 Mungu Amekuja ulimwenguni hasa kuzungumza maneno Yake; unachoshiriki nacho ni neno la Mungu, uonacho ni neno la Mungu, usikiacho ni neno la Mungu, unachokaa nacho ni neno la Mungu, unachopitia ni neno la Mungu, na Mungu aliyepata mwili huyu kimsingi hutumia neno kumfanya mwanadamu kamili. Yeye haonyeshi ishara na maajabu, na hasa hafanyi kazi ambayo Yesu Alifanya hapo awali. Ingawa wao ni Mungu, na wote ni mwili, huduma Zao sio sawa. Leo Mungu Amekuwa mwili kimsingi ili kukamilisha kazi ya “Neno kuonekana katika mwili,” kutumia neno kumfanya mwanadamu kamili, na kumfanya mwanadamu kukubali ushughulikiaji wa neno na usafishaji wa neno.

2 Katika maneno Yake, anakufanya kupata kupewa na kupata uzima; katika maneno Yake, unaona kazi Yake na matendo. Mungu Anatumia neno kukuadibu na kukutakasa, na hivyo ukipata ugumu wa maisha, ni pia kwa sababu ya neno la Mungu. Leo, Mungu hafanyi kazi kwa kutumia mambo ya hakika, ila ni kwa maneno. Baada tu ya neno Lake kuja juu yako ndipo Roho Mtakatifu Atafanya kazi ndani yako na kukufanya upate uchungu ama uhisi utamu. Ni neno la Mungu pekee ndilo linaloweza kukuleta katika hali halisi, na ni neno la Mungu pekee ndilo linaloweza kukufanya mkamilifu.

3 Kazi inayofanywa na Mungu katika siku za mwisho kimsingi ni kutumia neno Lake kumfanya kila mwanadamu kamili na kumwongoza mwanadamu. Kazi yote Anayofanya ni kupitia kwa neno; Hatumii ukweli kuadibu. Kuna wakati ambapo watu wengine humpinga Mungu. Mungu hasababishi ukosefu mkubwa wa starehe kwako, mwili wako hauadibiwi wala wewe kupitia ugumu—lakini pindi tu neno Lake linapokuja juu yako, na kukutakasa, hutaweza kuvumilia. Kwa hivyo, katika siku za mwisho, Mungu anapokuwa mwili, kimsingi Anatumia neno kukamilisha yote na kufanya yote yawe wazi.

Umetoholewa kutoka katika “Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 86 Mungu Anafanikisha Vyote Katika Siku za Mwisho Hasa Kwa Maneno

Inayofuata: 88 Mungu Mwenye Mwili Katika Siku za Mwisho Anafanya Kazi Zaidi Kutumia Maneno

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp