695 Mtazamo wa Petro kwa Majaribio

1 Mara nyingi Nilimweka chini ya jaribio, ambalo hakika lilimwacha nusu mfu, lakini hata katikati ya haya mamia ya majaribio, hakupoteza imani Kwangu hata mara moja ama kusikitishwa nami. Hata Niliposema nimemtupa kando, hakufa moyo wala kukata tamaa, lakini aliendelea kama mbeleni akitekeleza kanuni zake ili kunipenda kwa njia ya vitendo. Nilimwambia kwamba, ingawa alinipenda, Sikumsifu ila Ningemtupa katika mikono ya Shetani mwishowe. Katikati ya majaribio haya, ambayo hayakufikia mwili wake lakini yalikuwa majaribio ya njia ya maneno, bado alisali Kwangu.

2 “Ee, Mungu! Miongoni mwa mbingu na dunia na mambo lukuki, kuna mwanadamu yeyote, kiumbe chochote, ama kitu chochote kisicho mikononi Mwako, Mwenyezi? Unapotaka kunionyesha huruma, moyo wangu unafurahishwa sana na huruma Yako; unapotaka kunihukumu, ingawa sifai, nahisi hata zaidi siri ya kushangaza ya matendo Yako, kwa sababu Umejawa na mamlaka na hekima. Ingawa mwili wangu unapitia mateso, roho yangu ina faraja. Ningewezaje kutosifu hekima Yako na matendo Yako? Hata kama nitafa baada ya kuja kukujua, kamwe nitakuwa tayari.”

3 Katikati ya majaribu ya aina hizi, hata kama Petro hakuweza kufahamu nia Zangu kwa usahihi, ni wazi kwamba aliliona kuwa suala la fahari na utukufu binafsi kutumiwa na Mimi, na hakuwa mwenye huzuni kwa ajili ya kuwekwa chini ya jaribio. Kwa sababu ya uaminifu wake mbele Yangu, na kwa sababu ya baraka Zangu juu yake, amekuwa mfano mwema na mfano wa kuigwa kwa mwanadamu kwa maelfu ya miaka. Je, huui si hasa mfano unaopaswa kufuata? Wakati huu, unapaswa kufikiria sana na kujaribu kutatua mbona Nimepeana ripoti ndefu ya Petro. Hii inapaswa kukutumikia kama kanuni ya maadili.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 6” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 694 Ufahamu wa Petro Kuhusu Kuadibu na Hukumu

Inayofuata: 696 Lazima Ujue Jinsi ya Kupitia Kazi ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp