774 Maonyesho ya Petro ya Upendo kwa Mungu

1 Chochote katika maisha ya Petro ambacho hakikukimu mapenzi ya Mungu kilimfanya kuhisi wasiwasi. Kama hakikukidhi mapenzi ya Mungu, basi angehisi kujuta, na angetafuta njia mwafaka ambayo angejitahidi kuridhisha moyo wa Mungu. Hata katika masuala madogo kabisa maishani mwake yasiyokuwa na maana, bado alijishurutisha mwenyewe kukidhi mapenzi ya Mungu. Alikuwa pia mkali ilipofikia tabia yake ya asili na alikuwa daima mkali katika masharti yake mwenyewe ili kuelekea ndani zaidi kwa ukweli. Petro alimpenda Mungu hadi kiwango fulani, ambacho kilitakiwa na Mungu; ni watu kama hawa pekee wana ushuhuda.

2 Katika imani yake kwa Mungu, Petro alitafuta kumridhisha Mungu katika kila kitu, na alitafuta kutii yote yaliyotoka kwa Mungu. Bila malalamiko hata kidogo, aliweza kukubali kuadibu na hukumu, na vile vile usafishaji, dhiki na kuwa bila kitu maishani, yote ambayo hayangeweza kubadilisha upendo wake kwa Mungu. Je, huu haukuwa upendo mkamilifu kwa Mungu? Je, huku hakukuwa ni kutimiza wajibu wa kiumbe wa Mungu? Kuadibu, hukumu, dhiki—una uwezo wa kufikia utii hadi kifo, na hili ndilo linafaa kutimizwa na kiumbe wa Mungu, huu ni usafi wa upendo kwa Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 773 Uko Tayari Kumpa Mungu Upendo Ulio Moyoni Mwako

Inayofuata: 775 Tafuta Kumpenda Mungu Bila Kujali Mateso Yako Ni Makubwa Vipi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp