694 Ufahamu wa Petro Kuhusu Kuadibu na Hukumu

1 “Ni adabu ya Mungu na hukumu Yake ndiyo iliyoniokoa, na maisha yangu hayawezi kutengwa kutoka kwenye adabu na hukumu ya Mungu. Maisha yangu hapa duniani yamo chini ya himaya ya Shetani, na isingekuwa huduma na ulinzi na adabu ya Mungu na hukumu Yake, ningeliishi daima chini ya himaya ya Shetani, na, zaidi ya hayo, singekuwa na nafasi au njia ya kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana. Ni wakati tu ambapo adabu ya Mungu na hukumu kamwe hainiachi, ndio nitakapokuwa na uwezo wa kutakaswa na Mungu. Ni kwa maneno makali na tabia ya haki ya Mungu, na hukumu kuu ya Mungu, ndipo nimepata ulinzi mkuu, na kuishi katika mwanga, na kupokea baraka za Mungu. Kuwa na uwezo wa kutakaswa, na kujiweka huru kutokana na Shetani, na kuishi chini ya utawala wa Mungu—hii ndiyo baraka kubwa zaidi katika maisha yangu leo.”

2 Upendo wa Petro ulikuwa upendo safi. Huu ni ujuzi wa kufanywa mkamilifu, na ni ulimwengu wa juu wa kufanywa mkamilifu, na hakuna maisha yaliyo na maana zaidi ya haya. Alikubali adabu ya Mungu na hukumu, aliipenda tabia ya Mungu ya haki, na hakuna jambo kuhusu Petro lililokuwa la thamani zaidi ya hili. Alisema, “Shetani ananipa starehe za mwili, lakini mimi sithamini hayo. Adabu ya Mungu na hukumu inakuja juu yangu—na katika hili mimi nimeneemeka, katika hili mimi ninapata starehe, na katika hili mimi nimebarikiwa. Kama si kwa hukumu Yake, mimi singeweza kumpenda Mungu, bado ningeishi chini ya himaya ya Shetani, bado ningedhibitiwa nayo, na ningekuwa naamuriwa nayo. Kama ingekuwa vile, singewahi kuwa binadamu wa kweli, kwa maana singeweza kumtosheleza Mungu, na singejitoa kikamilifu kwa Mungu.

3 Japokuwa Mungu Hanibariki, na kuniacha bila faraja ndani yangu, kana kwamba moto mkuu unachoma ndani yangu, na hakuna amani au furaha, na hata ingawa adabu na nidhamu ya Mungu kamwe iko na mimi, katika adabu ya Mungu na hukumu ninao uwezo wa kuona tabia Yake ya haki. Mimi hupata furaha katika hili; hakuna kitu cha thamani zaidi au cha maana zaidi ya hili katika maisha. Ingawa ulinzi Wake na huduma vimekuwa adabu kali, hukumu, laana na mipigo, bado mimi hupata starehe katika mambo haya, kwani yanaweza kunitakasa bora zaidi na kunibadilisha, yanaweza kunileta karibu na Mungu zaidi, yanaweza kufanya niweze kumpenda Mungu zaidi, na yanaweza kufanya upendo wangu kwa Mungu uwe safi zaidi. Hii inanifanya niwe na uwezo wa kutimiza wajibu wangu kama kiumbe, na inanichukua mbele za Mungu na kuniweka mbali na ushawishi wa Shetani, ili nisije tena nikamtumikia Shetani.

Umetoholewa kutoka katika “Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 693 Mungu Hatimaye Huwapata wale Walio na Ukweli

Inayofuata: 695 Mtazamo wa Petro kwa Majaribio

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp