225 Kiini Cha Upinzani wa Mafarisayo kwa Yesu

1 Je, mngependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu? Je, mnataka kujua dutu ya Mafarisayo? Walikuwa wamejawa na mawazo makuu kuhusu Masiha. Kilicho zaidi, waliamini tu kuwa Masiha angekuja, ilhali hawakutafuta ukweli wa uzima. Na hivyo, hata leo bado wanamngoja Masiha, kwani hawana maarifa ya njia ya uzima, na hawajui ukweli ni nini. Ni vipi, hebu nielezeni, watu wapumbavu, wakaidi na washenzi kama hawa wangeweza kupata baraka za Mungu? Wangewezaje kumwona Masiha? Walimpinga Yesu kwa sababu hawakujua mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu, kwa sababu hawakuijua njia ya ukweli uliozungumziwa na Yesu, na zaidi, kwa sababu hawakumwelewa Masiha. Na kwa kuwa hawakuwa wamewahi kumwona Masiha na hawakuwa wamewahi kuwa pamoja na Masiha, walifanya kosa la kuning’inia bila mafanikio kwa jina la Masiha huku wakipinga dutu ya Masiha kwa kila njia iwezekanayo.

2 Mafarisayo hawa kwa dutu walikuwa wakaidi, wenye kiburi na hawakutii ukweli. Kanuni ya imani yao kwa Mungu ni: Haijalishi mahubiri Yako ni makubwa vipi, haijalishi mamlaka Yako ni makubwa vipi, Wewe si Kristo iwapo Huitwi Masiha. Je, maoni haya si ya upuuzi na ya kudhihaki? Je, si rahisi sana kwenu kufanya makosa ya Mafarisayo wa mbeleni zaidi, kwa kuwa hamna ufahamu hata kidogo kumhusu Yesu? Je, unaweza kuitambua njia ya ukweli? Je, unaweza kutoa uhakika kweli kuwa hutampinga Kristo? Je, una uwezo wa kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu? Kama hujui iwapo utampinga Kristo, basi Nasema kuwa tayari unaishi kwenye ukingo wa kifo.

Umetoholewa kutoka katika “Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 224 Wale Wasiokubali Ukweli Hawafai Kuokolewa

Inayofuata: 226 Utatu Upo?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp