432 Wacha Mungu ni Wale Walio Watulivu Mara Nyingi Mbele za Mungu

1 lazima kila mara uje mbele za Mungu, ule na unywe na kutafakari maneno Yake, na kukubali nidhamu na mwongozo Wake kwako. Lazima uweze kutii mazingira, watu, vitu, na mambo yote ambayo Mungu amekupangia, na inapofikia mambo ambayo huwezi kuyaelewa kabisa, lazima uombe mara kwa mara huku ukitafuta ukweli; unaweza kupata njia ya kusonga mbele kwa kuelewa tu mapenzi ya Mungu. Lazima umche Mungu, na ufanye kwa uangalifu kile unachopaswa kufanya; lazima mara nyingi uwe na amani mbele za Mungu, na usiwe mpotovu. Angalau, kitu kinapofanyika kwako, jibu lako la kwanza linapaswa kuwa kujituliza, na kisha uombe mara moja. Kwa kuomba, kungoja, na kutafuta, utapata ufahamu kuhusu mapenzi ya Mungu.

2 Ikiwa, ndani kabisa, wewe humcha Mungu na kumtii Mungu, na unaweza kuwa na utulivu mbele za Mungu na kufahamu mapenzi Yake, basi kwa kushirikiana na kutenda kwa njia hii, unaweza kulindwa. Hutakumbana na jaribu, au kumkosea Mungu, au kufanya vitu ambavyo vinakatiza kazi ya Mungu ya usimamizi, wala hutafika kiwango cha kuchochea chuki ya Mungu. Ikiwa moyo wako huishi mara nyingi mbele za Mungu, utazuiwa, na utamcha Mungu katika mambo mengi. Hutavuka mipaka, au kufanya chochote kilicho kiovu. Hutafanya kile kinachochukiwa na Mungu, wala hutasema maneno ambayo hayana maana. Ukikubali uchunguzi wa Mungu, na kukubali nidhamu ya Mungu, utaepuka kufanya mambo mengi maovu. Hivyo, si utakuwa umeepukana na uovu?

3 Who does not love the truth na humwombi Mungu au kutafuta ukweli jambo linapokutendekea, ikiwa mara kwa mara wewe hutenda kulingana na mapenzi yako, huishi kulingana na tabia yako ya shetani na kufichua tabia yako ya kiburi, na ikiwa hukubali uchunguzi wa Mungu au nidhamu ya Mungu, na humtii Mungu, basi watu kama hawa daima huishi mbele ya Shetani na hutawaliwa na tabia zao za shetani. Kwa hivyo watu kama hao hawana uchaji hata kidogo wa Mungu. Hawana uwezo kabisa wa kuepukana na uovu, na hata kama hawafanyi mambo maovu, kila kitu wanachofikiri bado ni kiovu, na hakihusiani na ukweli na kinakwenda kinyume cha ukweli. Wanafikiri kuwa ni haki yao kutenda uovu, na wao huchukulia imani katika Mungu kama aina ya maneno yanayorudiwarudiwa, kama aina ya utaratibu. Wao ni watu wasiomwamini Mungu!

Umetoholewa kutoka katika “Ukiiishi mbele ya Mungu Kila Wakati tu Ndio Unaweza Kuitembea Njia ya Wokovu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 431 Matokeo ya Kutuliza Moyo Wako Mbele za Mungu

Inayofuata: 433 Unapoutoa moyo wako kwa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp