543 Ikiwa Unaupenda Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kutenda Ukweli

1 Mbona ni vigumu sana kutafuta ukweli na kuuweka katika matendo jambo gumu sana—kana kwamba unaelekeza mashua dhidi ya mkondo, na lingeweza kurudi nyuma iwapo utaiacha kuielekeza mbele? Ni kwa sababu asili ya binadamu ni kumsaliti Mungu. Asili ya Shetani imechukua usukani wa kutawala ndani ya mwanadamu na hii ni nguvu ya kupinga. Wanadamu wenye asili ambayo inamsaliti Mungu bila shaka wana wepesi wa kufanya vitu vinavyomsaliti Yeye, na matendo mazuri kwa kawaida ni magumu kwao kutenda. Hii inaamuliwa kabisa na asili ya ubinadamu na kiini. Mara tu unapoelewa ukweli na unaanza kuupenda ukweli kutoka ndani yako mwenyewe, utakuwa na nguvu ya kufanya vitu vinavyopatana na ukweli. Hii kisha inakuwa kawaida, na hata bila juhudi na yenye kufurahisha, na unahisi kuwa kufanya chochote hasi kitahitaji juhudi za kiwango kikubwa. Hii ni kwa sababu ukweli umechukua utawala wa uongozi katika moyo wako.

2 Kama kweli unauelewa ukweli kuhusianana maisha ya mwanadamu, na kuhusu aina gani ya mtu wa kuwa—jinsi ya kuwa mtu wa tabia ya hali ya juu na wazi, mtu mwaminifu, mtu anayetoa ushuhuda kwa Mungu na kumtumikia Yeye—basi kamwe hutaweza kufanya tena mambo maovu ambayo Yanamkataa na kamwe hutachukua jukumu la kuwa kuongozi wa uongo, mfanyakazi wa uongo au mpinga Kristo. Hata kama Shetani akikudanganya, au mtu mwovu akikulazimisha, bado hutatenda kwa njia hiyo. Watu wanapopata ukweli na kuhisi chuki ndani kwa vitu hasi. Itakuwa vigumu kwao kutenda uovu, kwa sababu tabia yao ya maisha imebadilika na wamekamilishwa na Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Ni Kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 542 Ukweli wa Leo Unapewa Wale Wanaoutamani na Kuutafuta

Inayofuata: 544 Wale Wanaopenda Ukweli Watapata Ukweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp