501 Utendaji wa Kuacha Mwili
1 Jambo fulani linafanyika linalokutaka uvumilie hali ngumu, wakati huo unapaswa ufahamu ni nini mapenzi ya Mungu, na ni jinsi gani unapaswa kuyajali mapenzi ya Mungu. Usijiridhishe mwenyewe: Jiweke kando kwanza. Hakuna kitu kilicho duni kuliko mwili. Ni lazima udhamirie kumridhisha Mungu, na ni lazima utekeleze wajibu wako. Katika mawazo kama hayo, Mungu atakupa nuru ya kipekee katika jambo hili, na moyo wako pia utapata faraja. Jambo lolote likikutendekea, liwe dogo au kubwa, ni sharti kwanza ujiweke pembeni na kuuona mwili kama kitu duni zaidi kuliko vitu vyote. Kadiri unavyouridhisha mwili zaidi, ndivyo unavyochukua uhuru zaidi; ukiuridhisha mara hii, wakati mwingine utataka zaidi.
2 Mwili mara zote una tamaa kupita kiasi, kadiri unavyouridhisha mwili zaidi, ndivyo tamaa yake inaongezeka, na jinsi mwili unavyopotoka zaidi, hadi kufikia kiwango ambacho miili ya watu inahodhi dhana nzito, na kutomtii Mungu, na kujiinua, na kuanza kuishuku kazi ya Mungu. Miili ya wanadamu ni kama yule nyoka: asili yake ni kuyadhuru maisha yao—na ikipata mbinu yake kikamilifu, maisha yako yanapotea. Mwili ni wa Shetani. Kuna tamaa kupita kiasi ndani yake, hujithamini wenyewe, unafurahia faraja, na kushangilia burudani, kujiachilia katika uvivu na uzembe, na baada ya kuuridhisha kwa kiwango fulani mwishowe utakuangamiza.
Umetoholewa kutoka katika “Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli” katika Neno Laonekana katika Mwili