498 Ni Wale tu Wanaotenda Ukweli Ndio Wanaweza Kushuhudia Katika Majaribio

1 Kama unataka kuweza kusimama imara katika siku za usoni, kumridhisha vyema Mungu, na kumfuata hadi mwisho, unapaswa kujenga msingi thabiti leo, unafaa kumridhisha Mungu kwa kutia ukweli katika vitendo kwa kila jambo, na kuzingatia mapenzi Yake. Iwapo daima unatenda kwa namna hii, kutakuwa na msingi ndani yako, na Mungu atahamasisha ndani yako moyo unaompenda, na Atakupa imani. Siku moja ambapo majaribu yatakuwa yamekukumba kwa kweli, ijapo utaumia, na kuhisi umedhulumiwa kwa kiwango fulani, na kuwa na huzuni kubwa, kana kwamba ulikuwa umekufa—ila mapenzi yako kwa Mungu hayatabadilika, na yataongezeka zaidi. Hizo ni baraka za Mungu.

2 Ikiwa unaweza kumkubali Mungu na yote asemayo na atendayo leo kwa moyo mtiifu, basi kwa hakika utabarikiwa na Mungu, na kwa hivyo utakuwa mtu aliyebarikiwa na Mungu, na anayepokea ahadi Yake. Ikiwa leo hutendi, siku ambayo majaribu yatakukumba utakosa imani au moyo wenye mapenzi, na wakati huo jaribu litakuwa kishawishi; utatoswa ndani ya kishawishi cha Shetani na hutapata namna ya kuponyoka. Leo, unaweza kusimama imara jaribio dogo likikukabili, ila huenda usiweze kusimama imara siku ambayo jaribio kubwa litakukumba.

Umetoholewa kutoka katika “Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 497 Kutenda Ukweli Kunahitaji Gharama ya Kweli

Inayofuata: 499 Tenda Ukweli na Tabia Yako Itabadilika

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp