495 Tenda Ukweli Kwa Ajili ya Badiliko la Kweli

1 Kwa sasa, kuna mengi sana mnayopaswa kuingia kwayo na kutenda, na kwa sasa yana safu nyingi na maelezo ya kina. Kama huna ufahamu wa ukweli huu, ni thibitisho kwamba bado hujaingia. Mara nyingi, ufahamu wa mwanadamu kuhusu ukweli huwa wa juujuu; mwanadamu hushindwa kuweka ukweli wa kimsingi katika vitendo na hajui jinsi ya kushughulikia hata maswala madogo. Sababu ya mwanadamu kushindwa kutenda ukweli ni tabia yake ya uasi, na kwa sababu ufahamu wake kuhusu kazi ya sasa ni wa juu juu na wa kuegemea upande mmoja. Kwa hivyo, si kazi rahisi kwa mwanadamu kufanywa mkamilifu. Uasi wako ni wa hali ya juu sana, na unashikilia sana hali yako ya zamani; huwezi kusimama katika upande wa ukweli, na huwezi kutenda hata ukweli ulio wazi. Wanadamu kama hao hawawezi kuokolewa na ni wale ambao hawajashindwa.

2 Kama kuingia kwako hakuna kina au malengo, kukua kwako kutakujia polepole. Kama kuingia kwako hakuna uhalisi hata kidogo, basi kufuatilia kwako kutakuwa bure. Kama hujui kiini cha ukweli, hutabadilishwa. Ukuaji katika maisha ya mwanadamu na mabadiliko katika tabia zake hupatikana kwa kuingia ndani ya ukweli na, zaidi ya hili, kwa kuingia katika uzoefu wa kina. Ukiwa na uzoefu wa kina katika wakati wa kuingia kwako, na ukiwa na ufahamu halisi kuhusu kuingia, tabia yako itabadilika haraka. Ni baada ya kuangaziwa nuru na Roho Mtakatifu katika uzoefu wako ndipo utakapopata ufahamu wa kina kuhusu ukweli na uingie kwa kina.

Umetoholewa kutoka katika “Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 494 Uhalisi Huja tu kwa Kuyatenda Maneno ya Mungu

Inayofuata: 496 Tenda Ukweli Zaidi ili Kuendelea Zaidi Maishani

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp