103 Yasifu Maisha Mapya

Haleluya! Mwenyezi Mungu!

Tunakushukuru na kukusifu!

Haleluya! Mwenyezi Mungu!

Tunakuabudu Wewe milele!

1

Kristo ameonekana katika siku za mwisho.

(Haleluya! Halleluya!)

Maneno Yake yanatuhukumu, kututakasa na kutubadilisha.

(Haleluya! Halleluya!)

yakituongoza kwenye njia sahihi,

(Haleluya! Halleluya!)

naishi maisha mapya ya kumpenda Mungu.

(Haleluya! Halleluya!)

2

Ni ajabu kuuelewa ukweli.

(Haleluya! Halleluya!)

Naacha upotovu wangu na kujisikia huru kabisa.

(Haleluya! Halleluya!)

Dhana zangu zote zimeondoka,

(Haleluya! Halleluya!)

na uasi hauko ndani yangu tena.

(Haleluya! Halleluya!)

Hakuna kuzurura tena,

hakuna kuteseka tena.

Roho yangu imewekwa huru,

na ninaimba nikimsifu Mungu.

Ninaimba nikimsifu Mungu.

3

Upendo wa Mungu ni wa kweli na wa thamani,

(Haleluya! Halleluya!)

ukituongoza kwenye njia ing’aayo ya uzima.

(Haleluya! Halleluya!)

Nimeonja upendo mtamu sana.

(Haleluya! Halleluya!)

Nitampenda Mungu daima.

(Haleluya! Halleluya!)

4

Ndugu, dada, hebu tuje pamoja,

(Haleluya! Halleluya!)

bega kwa bega, pamoja kama kitu kimoja.

(Haleluya! Halleluya!)

Kwa moyo mmoja na nia moja,

(Haleluya! Halleluya!)

tunamtumikia na kuimba sifa Zake.

(Haleluya! Halleluya!)

Nani asiyeweza kusema kilicho moyoni mwake?

Nani asiyeweza kueleza upendo wake?

Unacheza na kumtukuza Mungu,

Ninapiga makofi kando yenu.

Ninapiga makofi kando yenu.

5

Nyimbo zetu zimejaa upendo kwa Mungu,

(Haleluya! Halleluya!)

kwa Mwenyezi Mungu tunafanywa upya.

(Haleluya! Halleluya!)

Maisha yetu potovu ya zamani yameisha,

(Haleluya! Halleluya!)

ni furaha kuishi mbele za Mungu!

(Haleluya! Halleluya!)

6

Kutenda ukweli kwa karibu kunatuweka huru;

(Haleluya! Halleluya!)

tunatimiza wajibu wetu na kumletea Mungu utukufu.

(Haleluya! Halleluya!)

Na watu wa Mungu wanafurahia maisha mapya,

(Haleluya! Halleluya!)

tunampenda Mungu na kuishi katika mwanga.

(Haleluya! Halleluya!)

Tumeivunja minyororo ya dunia,

tumeivunja minyororo ya familia,

tumeivunja minyororo ya mwili.

Jinsi gani ilivyo ya kupendeza kupendana!

Jinsi gani ilivyo ya kupendeza kupendana!

Iliyotangulia: 102 Mungu na Aguse Roho Zetu Mara Nyingine Tena

Inayofuata: 104 Naishi Katika Uwepo wa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp