312 Mungu Huwasifu Wale tu Wanaomtumikia Kristo kwa Shauku

1 Mnatamani sana kwa Mungu kufurahishwa nanyi, lakini bado mko mbali sana na Mungu. Tatizo ni nini hapa? Mnakubali tu maneno Yake, lakini sio ushughulikiaji na upogoaji Wake; hata zaidi hamwezi kukubali mpangilio Wake wote, kuwa na imani kamilifu Kwake. Tatizo, basi, ni gani hapa? Kimsingi, imani yenu ni kaka tupu la yai lisiloweza kutoa kifaranga. Kwani imani yenu haijawaletea ukweli ama kuwapa maisha, na badala imewaletea hisia danganyifu ya tumaini na msaada.

2 Madhumuni ya imani yenu kwa Mungu ni kwa ajili ya tumaini hili na msaada huu badala ya ukweli na maisha. Kwa hivyo, Nasema kwamba mkondo wa imani yenu kwa Mungu si mwingine bali ni kujaribu kujipendekeza kwa Mungu kupitia utumwa na kutokuwa na aibu, na hauwezi kuchukuliwa kuwa imani ya kweli hata kidogo. Kwa maneno mengine, ni tunda lipi ambalo imani kama hii inaweza kuzalisha? Azma ya imani yenu kwa Mungu ni kutimiza nia zenu kupitia kumtumia Mungu. Huu sio ukweli zaidi unaoonyesha kosa lenu dhidi ya tabia ya Mungu?

3 Mnaamini kuwepo kwa Mungu aliye mbinguni lakini mnakataa yule Mungu aliye duniani. Hata hivyo, Sikubaliani na maoni yenu. Nawapongeza tu wale wanadamu wanaosimama imara na kumtumikia Mungu wa duniani, kamwe sio wale wasiomkiri Kristo aliye duniani. Bila kujali jinsi wanadamu kama hawa walivyo waaminifu kwa Mungu aliye mbinguni, mwishowe, hawatauepuka mkono Wangu unaoadhibu waovu. Wanadamu kama hawa ni waovu; ni wale waovu wanaompinga Mungu na hawajawahi kumtii Kristo kwa furaha. Bila shaka, idadi yao inajumuisha wale wote wasiomjua na, zaidi, wasiomkiri Kristo.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 311 Mwanadamu Hana Imani ya Kweli Katika Kristo

Inayofuata: 313 Hakuna Amjuaye Mungu Mwenye Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp