7. Waumini katika Mungu Wanapasa Kujiandaa kwa Ajili ya Hatima Yao kwa Matendo Mema ya Kutosha

Maneno Husika ya Mungu:

Huruma Yangu inaonyeshwa kwa wale wanaonipenda Mimi na kujinyima. Kwa sasa, adhabu itakayowapata waovu, ni thibitisho hasa la tabia Yangu ya haki na, hata zaidi, ushuhuda wa hasira Yangu. Msiba utakapofika, wote wanaonipinga watalia watakapokumbwa na njaa na baa. Wale ambao wametenda aina zote za uovu, lakini ambao wamenifuata kwa miaka mingi, hawataepuka kulipia dhambi zao; wao pia, watatumbukia katika maafa, ambayo yameonekana kwa nadra kotekote katika mamilioni ya miaka, na wataishi katika hali ya taharuki na woga daima. Na wale kati ya wafuasi Wangu ambao wamekuwa waaminifu Kwangu watafurahi na kushangilia ukuu Wangu. Watakuwa na ridhaa isiyo na kifani na kuishi kwa raha ambayo Sijawahi kuwapa wanadamu. Kwa sababu Ninathamini matendo mema ya mwanadamu na kuchukia matendo yake maovu. Tangu Nilipoanza kuwaongoza wanadamu, Nimekuwa Nikitamani kwa hamu kupata kikundi cha watu ambao wanafikiria kama Mimi. Wale ambao hawana fikira sawa na Zangu, wakati ule ule, Siwasahau kamwe; Ninawachukia kabisa moyoni Mwangu daima, Nikisubiri nafasi ya kutoa adhabu kwao, jambo ambalo Nitafurahia kuona. Sasa siku Yangu imefika hatimaye, na Sihitaji kusubiri zaidi!

Kazi Yangu ya mwisho si kwa ajili ya kumwadhibu mwanadamu tu bali pia kwa ajili ya kupanga hatima ya mwanadamu. Aidha, ni kwa ajili ya kupokea shukrani kutoka kwa kila mtu kwa yale yote ambayo Nimefanya. Ninataka kila mtu aone kwamba yale yote ambayo Nimefanya ni sahihi na kwamba yote ambayo Nimefanya ni dhihirisho la tabia Yangu; si kwa uwezo wa mwanadamu, sembuse ulimwengu, ambao uliwaleta wanadamu. Kinyume na hili, mimi Ndiye Ninalisha kila kiumbe miongoni mwa vitu vyote. Bila uwepo Wangu, wanadamu wataangamia tu na kusumbuka kutokana na mashambulizi ya misiba. Hamna mwanadamu atakayeona uzuri wa jua na mwezi au dunia ya kijani kibichi; wanadamu watakumbana tu na usiku wenye baridi na bonde kali la uvuli wa mauti. Mimi tu Ndiye wokovu wa wanadamu. Mimi tu ndiye tumaini la wanadamu na zaidi ya hayo; Mimi tu Ndiye mwamba wa uwepo wa wanadamu wote. Bila Mimi, wanadamu watasimama kabisa mara moja. Bila mimi, wanadamu watakumbana na msiba mkuu na kukanyagwa na mapepo wa aina yote, hata kama hamna anayenisikiliza. Nimefanya kazi ambayo haiwezi kufanywa na yeyote yule ila mimi. tumaini Langu la pekee ni kwamba mwanadamu anaweza kunilipa kwa kutenda matendo kiasi mema. Ingawa wanaoweza kunilipa ni wachache, bado Nitahitimisha safari Yangu duniani na Nianze hatua ifuatayo ya kazi Yangu inayotokea, kwa sababu kukimbia kimbia Kwangu miongoni mwa wanadamu kwa miaka hii mingi imekuwa na matokeo mazuri, na Nimefurahishwa sana. Sijali kuhusu idadi ya watu ila kuhusu matendo yao mazuri. Kwa hali yoyote ile, Ninatumaini kwamba mtatayarisha matendo mema ya kutosha kwa ajili ya hatima yenu wenyewe. Huo ndio wakati Nitakaporidhika; la sivyo, hakuna yeyote miongoni mwenu atakayepuka maafa yatakayowafikia. Maafa haya hutoka Kwangu na bila shaka Mimi ndiye Niliyeyapanga. Ikiwa hamwezi kuonekana kuwa wema mbele Yangu, basi hamtaweza kuyaepuka maafa. Wakati wa majonzi, vitendo vyenu havikuchukuliwa kama vinavyofaa kabisa, kwa sababu imani na upendo wenu vilikuwa tupu, na mlijionyesha tu kuwa wenye woga au sugu. Kuhusu hili, Nitafanya hukumu ya mazuri au mabaya tu. Shaka Yangu inaendelea kuwa jinsi kila mmoja wenu hutenda na kujionyesha, kwa msingi ambao Nitatumia kufanya uamuzi kuhusu hatima yenu. Hata hivyo, ni sharti Niseme wazi kwamba: Sitawahurumia tena wale ambao hawakuwa waaminifu Kwangu kabisa wakati wa majonzi, kwa sababu huruma Yangu ina mipaka. Zaidi ya hayo, Simpendi yeyote yule ambaye amewahi kunisaliti Mimi, wala Sipendi kujihusisha na wale ambao hawawajali wenzao. Bila kujali huyo mtu ni nani, hii ndiyo tabia Yangu. Ni lazima Niwaambie hili: Yeyote atakayeuhuzunisha moyo Wangu hatapokea huruma kutoka Kwangu mara ya pili, na yeyote ambaye amekuwa mwaminifu Kwangu atadumu moyoni Mwangu milele.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako

Natarajia tu kuwa katika hatua ya mwisho ya kazi Yangu, mnaweza kutekeleza kwa kujitokeza, kujitoa kikamilifu, na wala sio shingo upande tena. Bila shaka, Natarajia pia kuwa nyote muwe na hatima nzuri. Hata hivyo, bado Nina mahitaji Yangu ambayo ni kwenu nyinyi mfanye uamuzi bora kabisa katika kujitoa Kwangu pekee na moyo wa ibada ya mwisho. Kama mtu hana moyo huo wa ibada pekee, mtu huyo hakika atakwenda kuwa thamani ya Shetani, na Mimi Sitaendelea kumtumia. Nitamtuma nyumbani akatunzwe na wazazi wake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Juu ya Hatima

Mnapaswa kufanya wajibu wenu wenyewe kwa kadri ya uwezo wenu kwa mioyo iliyo wazi na wima, na muwe tayari kufanya chochote kitakachohitajika. Kama mlivyosema, wakati siku itakuja, Mungu hatakosa kumjali mtu yeyote ambaye aliteseka au kulipa gharama kwa ajili Yake. Aina hii ya imani ni yenye thamani kuishikilia, na hampaswi kuisahau kamwe. Ni tu kwa njia hii Ninaweza kutuliza akili Yangu kuwahusu. Vinginevyo, Sitakuwa na uwezo wa kutuliza akili Yangu kuwahusu, na milele mtakuwa malengo ya chuki Yangu. Kama nyote mnaweza kufuata dhamiri zenu na kutoa yote kwa ajili Yangu, msiwache jitihada zozote kwa ajili ya kazi Yangu, na kutenga maisha ya jitihada za kazi ya injili Yangu, basi si moyo Wangu mara kwa mara utaruka kwa furaha kwa ajili yenu? Si Mimi Nitakuwa na uwezo wa kutuliza akili Yangu kuwahusu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Juu ya Hatima

Kama kutafuta njia ya ukweli kunakufurahisha vyema, basi wewe ni yule anayeishi kila mara katika mwangaza. Kama wewe unafurahia kuwa mtoa huduma katika nyumba ya Mungu, ukifanya kazi kwa bidii na kwa makini bila kuonekana, siku zote ukitoa na katu hupokei, basi Nasema kwamba wewe ni mtakatifu mwaminifu, kwani hutafuti tuzo na unakuwa tu binadamu mwaminifu. Kama uko radhi kuwa wazi, kama uko radhi kutoa kila kitu ulichonacho, kama una uwezo wa kujitolea maisha yako kwa ajili ya Mungu na kuwa shahidi, kama wewe ni mwaminifu hadi kwa kiwango ambapo unajua tu kumridhisha Mungu na si kujifikiria au kuchukua chochote kwa ajili yako, basi Nasema kwamba watu kama hao ndio wanaostawishwa na mwangaza na wataishi milele katika ufalme.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maonyo Matatu

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Matendo mema ni ushahidi kwamba tumepata wokovu, na ni dhihirisho la kuingia kwetu katika ukweli na uhalisi wa neno la Mungu. Kama tumetayarisha matendo mengi mema, hilo linamaanisha kwamba tumekuwa watu wapya mbele za Mungu na kwamba tuna ushahidi wa kweli katika kipengele cha kuwa binadamu halisi. Matendo yetu mema ndiyo yanayoonyesha hasa kwamba tumetubu kwa kweli; ikiwa tumetayarisha matendo mengi mema, hili linamaanisha kuwa tuna mfano wa kweli wa mtu. Ikiwa umemwamini Mungu kwa miaka mingi lakini umefanya matendo mema machache, basi una mfano wa binadamu? Je, una dhamiri na mantiki? Je, wewe ni mtu anayelipiza upendo wa Mungu? Iko wapi imani yako ya kweli? Uko wapi moyo wako wa upendo na utii kwa Mungu? Ni uhalisi upi umeingia ndani? Huna chochote kati ya haya. Kwa hiyo, mtu asiyefanya matendo mema ni mtu asiyepokea chochote kutoka kwa imani yake kwa Mungu. Yeye ni mtu ambaye hajapata kabisa wokovu kutoka kwa Mungu, mtu ambaye upotovu wake ni wa kina sana na ambaye hajabadilika hata kidogo. Matendo mema kweli yanafafanua hili.

Kimetoholewa kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha

Matendo mema ya kutosha ni yapi? Tunaweza kusema kwamba wajibu wowote ambao mtu anaweza au anapaswa kuutimiza katika uzoefu wake wa kazi ya Mungu, na kitu chochote ambacho Mungu anahitaji kutoka kwa mwanadamu—kama mwanadamu anaweza kufanya vitu hivi na anaweza kumridhisha Mungu, basi haya yote ni matendo mema Kama unaweza kuyatosheleza mahitaji ya Mungu, basi ni tendo jema. Kama una moyo wa ibada kwa Mungu wakati unapotimiza wajibu wako, basi ni tendo jema. Kama mambo unayoyafanya ni ya manufaa kwa watu waliochaguliwa na Mungu na kila mtu anafikiria kwamba unayoyafanya ni mazuri, basi ni tendo jema. Mambo yote ambayo dhamiri na mantiki ya mwanadamu huamini kuwa ni kulingana na madhumuni ya Mungu ni matendo mema. Mambo ambayo yanaweza kumridhisha Mungu na yana manufaa kwa watu wateule wa Mungu pia ni matendo mema. Kama mtu anaweza kufanya kila kitu ili kuyatayarisha haya matendo mema ambayo tumetoka kuzungumzia, hatimaye ataweza kuyatimiza, na hilo litamaanisha kuwa amekamilisha matendo mema ya kutosha. … Kila mtu sasa hutaka kutekeleza kazi yake na kufuatilia wokovu, lakini haitoshi tu kuwa na azimio na shauku. Mtu lazima aonyeshe tabia za utendaji na kuchukua hatua ya utendaji. Ni wajibu gani umetekeleza kwa ajili ya kuingia katika maisha ya watu wa Mungu wateule? Umefanya nini na ni thamani gani umelipa ili kuyaridhia matakwa ya Mungu? Umefanya nini ili kumridhisha Mungu na kulipa upendo Wake? Haya yote ni mambo ambayo inakubidi kuyatafakaria. Kama umefanya mambo mengi na kulipa thamani kubwa kwa ajili ya kuyaridhia matakwa ya Mungu na kwa ajili ya kuingia katika maisha na ukuaji wa watu wa Mungu wateule, basi inaweza kusemwa kuwa umeandaa matendo mema ya kutosha.

Kimetoholewa kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha

Kwa kiwango cha chini, kutimiza kazi kiasi haitoshi peke yake kufanyiza kiasi cha kuridhisha cha matendo mema. Hivyo ni kusema, kutekeleza tu kiasi kidogo cha wajibu wako hakufikiriwi kuwa matendo mema ya kuridhisha hata kidogo. Matendo mema ya kuridhisha bila shaka sio rahisi kama watu wafikiriavyo. Kuandaa kiasi cha kuridhisha cha matendo mema huhitaji kujitumia kabisa kwa ajili ya Mungu. Aidha, kunahitaji kulipa kila thamani, na kuwa mwaminifu kwa agizo la Mungu tangu mwanzo hadi mwisho kwa imani nzuri; hii ndiyo njia ya pekee ya kuyaridhia matarajio ya Mungu.

Katika kutimiza wajibu wao kuna watu ambao kweli wamelipa thamani, wakafanya mambo ambayo yamesifiwa na Mungu, ambao wametekeleza wajibu wao kwa njia ambazo ni nzuri kabisa, za ajabu, za kupendeza na za kufanikiwa sana kiasi kwamba wanaweza kufikiriwa kuwa wametekeleza matendo mema. Baadhi ya ndugu na dada wamekwenda jela kwa sababu ya kutekeleza wajibu wao, ambao wamepitia maumivu mengi makali bila kumtii Shetani, na wamekuwa mashahidi. Kisha kuna watu ambao huthubutu kujiingiza hatarini bila kujali usalama wa kibinafsi au manufaa, ambao wamejitolea kufanya kazi za hatari kwa roho ya kufanya lililo la haki kwa ujasiri. Na kuna wale ndugu na dada ambao wanaweza kujitolea kwa kazi ya injili, na wanaweza kuvumilia fedheha katika kuhubiri injili ili kuwaokoa watu. Pia kuna wale wenye bidii katika kazi ya injili, wakivumilia shida bila malalamiko, wakiweka kando mambo ya kibinafsi na ya familia huku mawazo yao yakijawa na jinsi wanavyoweza kueneza injili ili kuwaleta watu zaidi mbele ya Mungu na kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Wote ambao wamejitolea kujitumia kabisa ili kumridhisha Mungu ni wale watu ambao tayari wamefanya matendo mema. Lakini bado wana umbali fulani kutoka kwa “matendo mema ya kuridhisha” ambayo Mungu hutaka. Watu wengi wameandaa tu matendo mema kiasi na hawajayaridhia kabisa matakwa ya Mungu. Hilo linatuhitaji kufanya tunaloweza ili kutimiza wajibu wetu na tuwe na bidii katika kuingia ndani kabisa ya ukweli ili kutekeleza matendo mema ya kuridhisha. Hili linatuhitaji tutafute kufanikisha matokeo bora sana ili kuuridhisha moyo wa Mungu, bila kujali ni wajibu gani tunaoutimiza. Hasa katika kueneza injili, bila kujali jinsi fedheha tunayopitia ilivyo kubwa au ni mateso kiasi gani tunayoyavumilia, mradi tunaweza kuwaleta watu zaidi kupata wokovu, ni lazima tuuchukue kama wajibu bila kujali gharama za kibinafsi. Huku tu ndio kutekeleza tendo bora sana. Kama watu wanaweza kutekeleza matendo zaidi yaliyo mema kama hili, hayo yanaweza kufikiriwa kuwa matendo mema ya kuridhisha. Hilo ndilo humletea Mungu furaha na shangwe mno, na watu kama hao kwa hakika watapokea sifa za Mungu. Mbali na hili, katika kutimiza wajibu wetu ni lazima pia tuwe makini na waangalifu sana, daima tukitafuta kujiboresha, na kutojiruhusu kuzembea hata kidogo. Ili kujitumia kwa ajili ya Mungu, ni lazima tuwe na kujitolea kwa uaminifu kabla tuweze kuyaridhisha mapenzi ya Mungu kabisa.

Kimetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Iliyotangulia: 6. Maana ya Mateso na ni Mateso ya Aina Gani Ambayo Waumini wa Mungu Lazima Wastahimili

Inayofuata: Sura ya 8 Miisho ya Aina Mbalimbali za Watu na Ahadi ya Mungu kwa Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp