708 Mchakato wa Badiliko Katika Tabia
1 Mgeuzo wa tabia si badiliko katika matendo, si badiliko la nje lililobuniwa, si mgeuzo wa muda wa shauku, bali ni mgeuzo wa kweli wa tabia ambao huleta badiliko katika matendo. Mabadiliko kama hayo katika matendo ni tofauti kuliko mabadiliko katika mienendo ya nje. Mgeuzo wa tabia una maana kwamba umeelewa na umepitia ukweli, na kwamba ukweli umegeuka kuwa maisha yako. Zamani, ulifahamu ukweli kuhusu suala hili, lakini hukuweza kuchukua hatua kulihusu; kwako ukweli ulikuwa tu kama mafundisho ya dini yasiyodumu. Sasa, tabia yako imegeuka, na huelewi tu ukweli, lakini pia unatenda kulingana na ukweli.
2 Unaweza sasa kuacha vitu ambavyo ulikuwa unavipenda mno zamani; unaweza kuacha vitu ulivyokuwa radhi kufanya, mawazo yako mwenyewe, na fikira zako. Unaweza sasa kuacha vitu ambavyo hukuweza kuviacha zamani. Huu ni mgeuzo wa tabia na ni mchakato wa kuigeuza tabia yako. Inasikika kuwa rahisi kabisa, lakini kwa kweli, mtu aliye katikati ya hilo lazima apitie shida nyingi, aushinde mwili wake na aache mambo ya mwili wake ambayo ni ya asili yake. Lazima pia apitie kushughulikiwa na kupogolewa, kuadibu na hukumu, na lazima apitie majaribio. Ni baada ya kupitia haya yote tu ndio mtu anaweza kuifahamu asili yake. Kuwa na ufahamu kiasi hakumaanishi kwamba anaweza kubadilika mara moja. Lazima apitie shida katika mchakato huo.
Umetoholewa kutoka katika “Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo