Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

702 Unalindwa Kwa Sababu Unaadibiwa na Kuhukumiwa

1 Leo, ni kwa sababu ninyi huadibiwa, hulaaniwa, na huhukumiwa ndipo ninyi hupewa ulinzi. Ni kwa sababu mmepitia mengi ndipo ninyi hulindwa. La sivyo, mngekuwa mmetumbukia katika uharibifu zamani. Sifanyi mambo yawe magumu kwenu kwa kudhamiria—asili ya mwanadamu imefanywa madhubuti kwa imara, na lazima iwe hivi ili tabia za watu zibadilishwe. Leo, ninyi hamna hata urazini au kujitambua kwa Paulo, wala hamna dhamiri yake. Ninyi kila mara lazima mshurutishwe, na ninyi kila mara lazima muadibiwe na kuhukumiwa ili kuamsha roho zenu. Kuadibu na hukumu ndivyo vilivyo bora zaidi kwa maisha yenu. Na kama inabidi, lazima pia kuwe na kuadibu kwa ufikaji wa ukweli; ni wakati huo tu ndipo utatii kwa ukamilifu.

2 Asili zenu ni kiasi kwamba bila kuadibu na laana, mngekuwa hamko radhi kuinamisha vichwa vyenu, mngekuwa hamko radhi kutii. Bila ukweli mbele ya macho yenu, hakungekuwa na athari. Ninyi ni duni mno na wasio thamani katika hulka! Bila kuadibu na hukumu, ingekuwa vigumu ninyi kushindwa, na vigumu kwa udhalimu na kutotii kwenu kukomeshwa. Asili yenu ya zamani imekita mizizi sana. Kama mngewekwa juu ya kiti cha enzi, hamngekuwa na habari kuhusu kimo cha mbingu na kina cha dunia, sembuse mlikokuwa mkielekea. Ninyi hata hamjui mlikotoka, kwa hiyo mngemjuaje Muumba?

3 Bila kuadibu na laana ya wakati wa kufaa ya leo, siku zenu za mwisho zingekuwa zimefika kitambo. Sembuse majaliwa yenu—hilo haliko hatarini hata zaidi? Bila kuadibu na hukumu hii ya wakati wa kufaa, nani ajuaye vile mngekuwa wenye kiburi, na nani ajuaye vile mngekuwa wapotovu. Hamna uwezo wowote wa kudhibiti na kutafakari kuhusu ninyi wenyewe. Kuadibu huku na hukumu imewafikisha leo, na imehifadhi kuishi kwenu. Hampaswi kutenda bora zaidi katika kukubali kuadibu na hukumu ya leo? Ni machaguo gani mengine mliyonayo?

Umetoholewa kutoka katika “Utendaji (6)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia:Pitia Hukumu ya Mungu ili Utupilie Mbali Ushawishi wa Shetani

Inayofuata:Hukumu ya Mungu Hufichua Haki na Utakatifu Wake

Maudhui Yanayohusiana

 • Kwa Kuwa Mungu Anamwokoa Mwanadamu, Atamwokoa Kabisa

  1 Kwa kuwa Mungu alimwokoa mwanadamu, Atamwongoza; kwa kuwa Anamwokoa mwanadamu, Atamwokoa na kumpata kabisa; kwa kuwa anamwongoza mwanadamu, Atamfiki…

 • Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote

  1 Kutoka unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutenda wajibu wako. Katika mpango na utaratibu wa Mungu, unachukua nafasi yako, na unaanza safar…

 • Umuhumi wa Maombi

  1 Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo utakavyoguswa zaidi, ku…

 • Umuhimu wa Mungu Kumsimamia Binadamu

  Usimamizi wa Mungu ni ili kuwapata binadamu wanaomwabudu na kumtii Yeye. Ingawa wamepotoshwa na Shetani, hawamwiti baba tena, hawamwiti baba tena. 1 …