819 Unajua Kusudi na Maana ya Kazi ya Mungu?

1 Sasa unajua kweli ni kwa nini unaniamini Mimi? Kweli unajua kusudi na umuhimu wa kazi Yangu? Kweli unajua wajibu wako? Kweli unaujua ushuhuda Wangu? Kama unaniamini Mimi tu, ilhali si utukufu Wangu wala ushuhuda Wangu vinaweza kuonekana ndani yako, basi Nimekutupa nje kitambo kirefu. Kwa wale wanaoona wanajua kila kitu, wao ni miiba zaidi katika macho Yangu, na katika nyumba Yangu, wao ni vizuizi tu Kwangu. Wao ndio magugu yanayopaswa kupepetwa kabisa na kuondolewa kwenye kazi Yangu, bila ya jitihada hata kidogo na bila ya uzito wowote; Nimevichukia kitambo kirefu.

2 Na kwa wale bila ya ushuhuda, hasira Yangu siku zote iko juu yao, na kiboko Changu hakijawahi kutoka kwao. Kitambo kirefu Nimewakabidhi kwenye mikono ya yule mwovu, na hawana tena baraka Zangu zozote. Na siku hiyo ikifika, adhabu yao itakuwa mbaya zaidi kuliko ile ya wanawake wajinga. Sasa hivi Ninafanya kazi ile ambayo ndiyo wajibu Wangu kufanya; Nitakusanya pamoja ngano yote, pamoja na magugu. Hii ndiyo kazi Yangu sasa. Magugu haya yataweza kupepetwa na kuondolewa wakati wa kupepeta Kwangu, kisha nafaka za ngano zitakusanywa kwenye ghala, na magugu ambayo yatakuwa yamepepetwa yatawekwa motoni na kuchomwa hadi kugeuka jivu.

3 Kazi Yangu sasa ni kuwaweka tu binadamu wote kwa pamoja, yaani, kuweza kuwashinda wote kabisa. Kisha Nitaanza upepetaji wa kufichua mwisho wa binadamu wote. Kwa hiyo unastahili kujua namna ya kunitosheleza Mimi sasa na namna unavyostahili kuwa kwenye njia iliyo sawa katika imani yako Kwangu. Kile Ninachotafuta ni uaminifu na utiifu wako sasa, upendo wako na ushuhuda wako sasa. Hata kama hujui kwa wakati huu kile ambacho ushuhuda unamaanisha au kile ambacho upendo unamaanisha, unafaa kuniletea kila kitu, na kunikabidhi mimi hazina za pekee ulizonazo: uaminifu na utiifu wako.

Umetoholewa kutoka katika “Unajua Nini Kuhusu Imani?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 818 Uko Tayari Kuwa Mtu Anayemshuhudia Mungu?

Inayofuata: 820 Ushuhuda Anaopaswa Kuwa Nao Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp