164 Sababu Ya Kupata Mwili Kwa Mungu katika Siku za Mwisho

1 Katika siku za mwisho, Mungu alipata mwili ili kufanya kazi Aliyopaswa kufanya na kutekeleza huduma Yake ya maneno. Alikuja yeye mwenyewe ili kufanya kazi kati ya wanadamu kwa lengo la kuwakamilisha wale watu ambao wanaipendeza nafsi Yake. Kutoka wakati wa uumbaji hadi leo Yeye hufanya tu hiyo kazi wakati wa siku za mwisho. Ni wakati wa siku za mwisho tu ambapo Mungu alipata mwili ili kufanya kazi kwa kiwango kikubwa. Ingawa Yeye huvumilia shida ambazo watu wanaweza kupata ugumu kuvumilia, ingawa Yeye kama Mungu mkuu ana unyenyekevu wa kuwa mtu wa kawaida, hakuna kipengele cha kazi Yake kimecheleweshwa, na mpango Wake haujatupwa katika mchafuko hata kidogo. Anafanya kazi kulingana na mpango Wake wa awali.

2 Mojawapo ya madhumuni ya kupata mwili huku ni kuwashinda watu. Mengine ni kuwakamilisha watu Anaowapenda. Yeye hutamani kuwaona kwa macho Yake mwenyewe watu Anaowakamilisha, na Yeye hutaka kujionea Mwenyewe jinsi watu Anaowakamilisha humshuhudia. Sio mtu mmoja ambaye hukamilishwa, na sio wawili. Hata hivyo, ni kikundi cha watu wachache sana. Kikundi hiki cha watu huja kutoka nchi mbalimbali za dunia, na kutoka kwa makabila mbalimbali ya ulimwengu. Kusudi la kufanya kazi hii nyingi ni kukipata kikundi hiki cha watu, kupata ushuhuda ambao kikundi hiki cha watu humtolea, na kupata utukufu ambao Yeye hupata kupitia kwa kikundi hiki cha watu.

Umetoholewa kutoka katika “Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaoweza Kukamilishwa” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 163 Sababu ya Kristo Kuja Kufanya Kazi Duniani

Inayofuata: 165 Hakuna Anayejua Kuhusu Kufika kwa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp