400 Ufuatiliaji Unaopaswa Kufuatwa na Waumini

1 Je, ni nini unachopaswa kufuatilia sasa? Iwapo unaweza kushuhudia kazi ya Mungu au la, iwapo unaweza kuwa ushuhuda na udhihirisho wa Mungu au la, na iwapo unastahili kutumiwa na Yeye au la—hivi ndivyo vitu unavyopaswa kutafuta. Ni kiasi gani cha kazi ambacho Mungu hakika amefanya kwako? Ni kiasi gani ambacho umeona, ni kiasi gani ambacho umegusa? Umepitia kiasi gani, na kuonja kiasi gani? Bila kujali iwapo Mungu amekujaribu, kukushughulikia, au kukuadhibu, matendo Yake na kazi Yake vimetekelezwa juu yako. Lakini kama muumini katika Mungu na kama mtu ambaye ana nia ya kufuatilia kukamilishwa na Yeye, je, unaweza kushuhudia kazi ya Mungu kwa msingi wa uzoefu wako wa vitendo? Je, unaweza kuwakimu wengine kupitia uzoefu wako mwenyewe wa vitendo, na kutumia maisha yako yote kushuhudia kazi ya Mungu? Ili kushuhudia kazi ya Mungu, lazima utegemee uzoefu na maarifa yako, na gharama ambayo umelipa. Kuwaruhusu watu wajue kazi Yake na kuona matendo Yake. Kama kweli unatafuta yote haya, basi Mungu atakukamilisha.

2 Ikiwa yote unayotafuta ni kukamilishwa na Mungu na kubarikiwa mwishoni kabisa, basi mtazamo wa imani yako katika Mungu si safi. Unapaswa kuwa ukifuatilia jinsi ya kuona matendo ya Mungu katika maisha ya kweli, jinsi ya kumridhisha Yeye Anapokufichulia mapenzi Yake, na kutafuta jinsi unavyopaswa kushuhudia maajabu na hekima Yake, na jinsi ya kushuhudia jinsi Anavyokufundisha nidhamu na kukushughulikia. Haya yote ni mambo unayopaswa kuwa ukiyatafakari sasa. Kama upendo wako kwa Mungu ni ili tu uweze kushiriki katika utukufu wa Mungu baada ya Yeye kukukamilisha, basi bado hautoshi na hauwezi kukidhi mahitaji ya Mungu. Unahitaji kuwa na uwezo wa kushuhudia kazi ya Mungu, kutosheleza mahitaji Yake, na kuwa na uzoefu wa kazi ambayo Amefanya kwa watu kwa njia ya utendaji. Iwe ni uchungu, majonzi, au huzuni, lazima upitie vitu hivi vyote katika kutenda kwako. Vitu hivi vinanuiwa kukukamilisha kama Yule anayemshuhudia Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Wale Wanaopaswa Kukamilishwa Lazima Wapitie Usafishaji” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 399 Njia ya Kumwaamini Mungu Ndiyo Njia ya Kumpenda

Inayofuata: 401 Umuhimu wa Kumwamini Mungu ni Mkubwa Sana

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp