664 Mungu Anapoijaribu Imani ya Binadamu

1 Nikiiweka imani ya binadamu katika majaribu, hakuna hata mwanadamu mmoja aliye na uwezo wa kuwa na ushuhuda wa kweli, hakuna hata mmoja anayeweza kujitoa kikamilifu; badala yake, mwanadamu anashinda akijificha na kukataa kujifungua na kuwa wazi, kana kwamba Ninaenda kuupora moyo wake. Hata Ayubu hakustahimili majaribu, wala hakufurahia katika mateso. Watu wote wanatoa dokezo iliyofifia ya kijani kibichi katika joto la majira ya kuchipua; wao hawasalii kwenye hali ya kijani kibichi chini ya mlipuko wa baridi wa majira ya baridi. Akiwa mwenye mifupa na mkonde na gofu kwa kimo, mwanadamu hawezi kutimiza nia Zangu.

2 Katika binadamu wote, hakuna hata mmoja anayeweza kutumika kuwa mfano kwa wengine, kwa sababu wanadamu ni sawa tu, bila tofauti kati yao, na kuna kidogo kinachowatofautisha mmoja na mwingine. Kwa sababu hii, hata leo wanadamu bado hawana uwezo wa kuijua kazi Yangu. Ni wakati ambao kuadibu Kwangu kutawashukia wanadamu ndipo wanadamu, bila kujua, wataifahamu kazi Yangu, na bila Mimi kufanya lolote ama kumlazimisha yeyote, wanadamu watakuja kunijua, na hivyo kupata kuiona kazi Yangu. Huu ni mpango Wangu, ni kipengele cha kazi Yangu ambayo ni wazi, na ni kile mwanadamu lazima afahamu.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 26” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 663 Unapaswa Kusimama Upande wa Mungu Majaribio Yafikapo

Inayofuata: 665 Anachotaka Mungu Katika Majaribio Ni Moyo wa Kweli wa Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp