425 Wale Tu Walio Watulivu Mbele Ya Mungu Ndio Wanaolenga Maisha

1 Mtu anayeweza kuwa mtulivu kwa kweli mbele ya Mungu anaweza kujiachilia huru kutoka kwa vifungo vyote vya kidunia na anaweza kutimiza kumilikiwa na Mungu. Watu wote wasioweza kutulia mbele ya Mungu ni wafisadi na wasiozuiwa kwa yakini. Wale wote wanaoweza kutulia mbele ya Mungu ni watu ambao ni wacha Mungu mbele ya Mungu, watu wanaomtamani Mungu.

2 Ni watu walio watulivu tu mbele ya Mungu ndio wanaotilia maanani maisha, wanaotilia maanani ushirika katika roho, walio na kiu ya maneno ya Mungu, na wanaofuatilia ukweli. Wale wote wasiotilia maanani kutulia mbele ya Mungu, wasiofanya mazoezi ya kuwa watulivu mbele ya Mungu ni watu ovyo ambao wamejifunga kabisa kwa dunia, wasio na uzima; hata wakisema wanaamini katika Mungu wanaunga mkono kwa maneno matupu tu.

3 Wale ambao Mungu hukamilisha na kufanya kamili hatimaye ni watu wanaoweza kuwa watulivu mbele ya Mungu. Kwa hivyo, watu walio watulivu mbele ya Mungu ni watu walioneemeshwa na baraka nyingi. Watu ambao mchana hutumia muda mchache kula na kunywa maneno ya Mungu, ambao wameshughulika kabisa na mambo ya nje, na hawatilii maanani kuingia katika uzima wote ni wanafiki wasiokuwa na matarajio ya kuendelea katika siku za usoni. Ni wale wanaoweza kutulia mbele ya Mungu na kushiriki kwa uhalisi na Mungu ndio watu wa Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Kuhusu Kuutuliza Moyo Wako Mbele ya Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 424 Kumtumainia na Kumtegemea Mungu ni Hekima Kubwa Zaidi

Inayofuata: 426 Unapaswa Kujitahadhari Kutuliza Moyo Wako Mbele za Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp