431 Matokeo ya Kutuliza Moyo Wako Mbele za Mungu

1 Kuja mbele ya Mungu kukubali maneno Yake kama uzima wako, lazima kwanza uwe mtulivu mbele ya Mungu. Ni wakati unapokuwa tu mtulivu mbele ya Mungu ndio Mungu atakupa nuru na kukufanya uelewe. Kadri watu wanavyokuwa watulivu zaidi mbele ya Mungu, ndivyo wanavyoweza kupata nuru na mwangaza wa Mungu zaidi. Haya yanawahitaji watu kuwa na uchaji Mungu na imani. Ni hivyo tu ndivyo wanaweza kutimiza ukamilifu. Zoezi la msingi la kuingia katika maisha ya kiroho ni kuwa mtulivu mbele ya Mungu. Mazoezi yako yote ya kiroho yatafaa tu ikiwa unatulia mbele ya Mungu. Ikiwa huwezi kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu huwezi kupokea kazi ya Roho Mtakatifu. Kusudi la kuwa mtulivu mbele ya Mungu ni kuwa mwenye ari na wa vitendo na kutafuta usahihi na uangavu katika maneno ya Mungu, hatimaye kutimiza kufahamu ukweli na kumjua Mungu.

2 Ikiwa tu mmetulia kwa kweli mbele ya Mungu ndipo mtaelewa kuhusu maneno ya sasa ya Mungu, kutenda kwa usahihi zaidi mwanga na kupata nuru kwa Roho Mtakatifu na kutopotoka, kuweza kuelewa dhahiri zaidi makusudi ya Mungu na kuwa na mwelekeo wazi zaidi katika huduma yako, kuweza kuelewa kwa usahihi zaidi mguso na uongozi wa Roho Mtakatifu na kuwa na uhakika wa kuishi chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. Haya ndiyo matokeo ambayo kuwa mtulivu kwa kweli mbele ya Mungu hutimiza. Wakati watu hawaelewi kuhusu maneno ya Mungu, hawana njia ya kutenda, hawawezi kuyaelewa makusudi ya Mungu, au hawana kanuni za kutenda, hii ni kwa sababu mioyo yao haijatulia mbele ya Mungu. Kusudi la kuwa mtulivu mbele ya Mungu ni kuwa mwenye ari na wa vitendo na kutafuta usahihi na uangavu katika maneno ya Mungu, hatimaye kutimiza kufahamu ukweli na kumjua Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Kuhusu Kuutuliza Moyo Wako Mbele ya Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 430 Desturi wa Kuwa Mtulivu Mbele Ya Mungu

Inayofuata: 432 Wacha Mungu ni Wale Walio Watulivu Mara Nyingi Mbele za Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp