489 Soma Maneno ya Mungu Kuhusiana na Hali Zako

1 Unapokula na kunywa maneno ya Mungu, lazima utathmini uhalisi wa hali yako mwenyewe kulingana na vitu hivi. Yaani, unapogundua dosari zako wakati wa uzoefu wako wa kweli, lazima uweze kupata njia ya kutenda, uweze kupuuza nia na fikira zako zisizo sahihi. Ukijitahidi daima kupata vitu hivi na utake kuvitimiza kwa dhati, basi utakuwa na njia ya kufuata, hutahisi mwenye utupu, na hivyo utaweza kudumisha hali ya kawaida. Ni hapo tu ndipo utakuwa mtu anayebeba mzigo katika maisha yako mwenyewe, aliye na imani.

2 Mbona watu wengine hawawezi kuyaweka maneno ya Mungu katika vitendo baada ya kuyasoma? Je, si kwa sababu hawayachukulii maisha kwa uzito? Sasabu ya wao kutoelewa vitu muhimu na kukosa njia ya kutenda ni kuwa wanaposoma maneno ya Mungu, hawawezi kuyahusisha na hali zao wenyewe, wala hawawezi kuwa na ujuzi wa hali zao wenyewe. Jinsi ya kuweka kando raha za mwili, jinsi ya kuweka kando kujidai, jinsi ya kujibadili, jinsi ya kuviingia vitu hivi, jinsi ya kuboresha ubora wako wa tabia, na kuanzia kutoka kipengele kipi. Unaelewa tu mambo machache ya nje, na yote unayoyajua ni kwamba kweli umepotoka sana. Kwa kweli, tabia yako potovu haijabadilika, jambo linalothibitisha kwamba hujapata njia ya kutenda.

3 Anza kujifunza hivi: Kwanza, yasome maneno ya Mungu, pata kujua vyema maneno ya kiroho yaliyo ndani yake; pata maono muhimu yaliyo ndani yake; tambua sehemu zinazohusu utendaji; viunganishe pamoja vitu hivi, moja baada ya kingine; viingie katikati ya uzoefu wako mwenyewe. Hivi ndivyo vitu muhimu unavyopaswa kuelewa. Utendaji muhimu zaidi wakati wa kula na kunywa maneno ya Mungu ni huu: Baada ya kusoma sura ya maneno ya Mungu, ni lazima uweze kutambua sehemu muhimu zinazohusu maono, na pia ni lazima uweze kutambua sehemu muhimu zinazohusu utendaji; tumia maono kama msingi, na utumie utendaji kama mwongozo wako maishani.

Umetoholewa kutoka katika “Utendaji (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 488 Jinsi ya Kuingia Katika Uhalisi wa Maneno ya Mungu

Inayofuata: 490 Fanya Jitihada Katika Kutenda Kwako Neno la Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp