494 Uhalisi Huja tu kwa Kuyatenda Maneno ya Mungu

1 Kazi na neno la Mungu vinanuiwa kusababisha badiliko katika tabia yenu; lengo Lake si tu kuwafanya muelewe ama mjue kazi na neno Lake. Hilo halitoshi. Ni lazima watu wapitie vipengele vyote vya ukweli kwa utondoti, na wauchunguze na kuutafuta kwa kina zaidi, badala ya kusubiri tu kufyonza chochote wanachopewa. Wanajua neno la Mungu, lakini hawaliweki katika vitendo. Mtu wa aina hii hapendi ukweli na mwishowe ataondolewa. Ili kuwa kama Petro wa miaka ya tisini, hili linamaanisha kwamba kila mmoja wenu anapaswa kutenda neno la Mungu, aingie kwa kweli katika yale unayoyapitia na apate nuru hata zaidi na kubwa zaidi katika ushirikiano wake na Mungu, ambao utakuwa wa msaada unaozidi daima kwa maisha yenu mwenyewe.

2 Ikiwa mmesoma maneno mengi ya Mungu lakini mnaelewa tu maana ya maandiko na hamna maarifa ya moja kwa moja ya neno la Mungu kupitia uzoefu wenu halisi, basi hutajua neno la Mungu. Kwa kadiri inavyokuhusu, neno la Mungu si uzima, bali tu nyaraka zisizovutia. Na ikiwa unaishi tu kwa kufuata nyaraka zisizovutia, basi huwezi kuelewa asili ya neno la Mungu wala hutaelewa mapenzi Yake. Ni wakati tu ambapo unapitia neno Lake katika matukio yako halisi ndipo maana ya kiroho ya neno la Mungu itafichuka kwako, na ni kupitia uzoefu tu ndiyo unaweza kuelewa maana ya kiroho ya ukweli mwingi na ufungue siri za neno la Mungu.

3 Usipouweka katika vitendo, basi bila kujali jinsi neno Lake lilivyo dhahiri, yote uliyoelewa ni nyaraka na mafundisho matupu tu, ambayo yamekuwa kanuni za kidini kwako. Je, Mafarisayo hawakufanya hivi? Kwa kweli, mchakato wa kumwamini Mungu ni mchakato wa ninyi kupitia neno Lake na vilevile kupatwa na Yeye, ama kuzungumza dhahiri zaidi, kumwamini Mungu ni kuwa na maarifa na ufahamu wa neno Lake na kupitia na kuishi kwa kudhihirisha neno Lake; huu ndio uhalisi wa ninyi kumwamini Mungu. Ikiwa mnamwamini Mungu na mnatumai kupata uzima wa milele bila kutafuta kutenda neno la Mungu kama kitu kilicho ndani yenu, basi ninyi ni wapumbavu.

Umetoholewa kutoka katika “Punde Unapoelewa Ukweli, Unapaswa Kuuweka Katika Vitendo” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 493 Ungependa Kuwa Tunda la Kufurahiwa na Mungu?

Inayofuata: 495 Tenda Ukweli Kwa Ajili ya Badiliko la Kweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp