652 Ninyi Ndio Wale Watakaopokea Urithi wa Mungu

1 Kama mtu anayemwamini Mungu, inakupasa kuelewa kuwa, leo, katika kupokea kazi ya Mungu nyakati za mwisho na kazi yote ya mpango wa Mungu ndani yako, umepokea utukufu mkuu na wokovu wa Mungu kabisa. Kazi yote ya Mungu ulimwengu mzima imelenga watu wa kikundi hiki. Amejitolea kwa nguvu Zake zote na kutoa vyote kwa ajili yako; Amekurejesha na kukupa kazi yote ya Roho ulimwenguni kote. Ndiyo sababu Nasema kuwa wewe una bahati. Kwa hiyo, ninyi ndio mtakaopokea urithi wa Mungu, na hata zaidi warithi wa utukufu wa Mungu.

2 Pengine utayakumbuka maneno haya: “Kwa kuwa huzuni yetu nyepesi, ambayo ni ya muda mdogo pekee, inatufanyia utukufu mkubwa na wa daima ambao unazidi kuwa mkuu kabisa.” Maneno haya ndiyo yatakayotimizwa na Mungu katika enzi za mwisho. Yatatimia kwa wale walioteswa na joka kuu jekundu katika sehemu linakoishi. Joka kuu jekundu humtesa Mungu na ni adui wa Mungu, kwa hiyo katika nchi hii, wanaomwamini Mungu wanateswa na kudhihakiwa. Ndiyo sababu maneno haya yatakuja kuwa kweli kwenu nyie kundi la watu.

3 Ni vigumu kabisa kwa Mungu kutekeleza kazi yake katika nchi yenye joka kuu jekundu, lakini ni kupitia ugumu huu ndipo Mungu Hupiga hatua katika kazi Yake ili kudhihirisha hekima Yake na matendo Yake ya ajabu. Mungu Huchukua fursa hii kuwakamilisha watu hawa wa kikundi hiki. Kwa ajili ya mateso ya watu, tabia yao na hulka ya kishetani ya watu katika nchi hii najisi, Mungu Anafanya kazi Yake ya kutakasa na ushindi, ili, kutokana na hili, apokee utukufu na kuwapata wale wote wanaoshuhudia matendo Yake. Huu ndio umuhimu wa kujitoa kwa Mungu kwa ajili ya kikundi hiki cha watu.

Umetoholewa kutoka katika “Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Kama Vile Mwanadamu Anavyodhania?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 651 Kupitia Shida Kuna Umuhimu Mkubwa

Inayofuata: 653 Jinsi ya Kukubali Hukumu ya Maneno ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp