679 Usafishaji Ndiyo Mbinu Bora ya Mungu Kumkamilisha Mwanadamu

1 Kadiri usafishaji wa Mungu ulivyo mkubwa, ndivyo mioyo ya watu inaweza kumpenda Mungu zaidi. Mateso ndani ya mioyo yao ni ya manufaa kwa maisha yao, wanaweza zaidi kuwa na amani mbele ya Mungu, uhusiano wao na Mungu ni wa karibu zaidi, na wanaweza kuona vizuri zaidi upendo wa juu kabisa wa Mungu na wokovu Wake wa juu kabisa. Petro alipitia usafishaji mamia ya mara, na Ayubu alipitia majaribio kadhaa. Ikiwa mngependa kufanywa kamili na Mungu, nyinyi pia sharti mpitie usafishaji mamia ya mara; ni ikiwa tu mtapitia mchakato huu, na mtegemee hatua hii, ndiyo mnaweza kuridhisha mapenzi ya Mungu, na kufanywa kamili na Mungu.

2 Usafishaji ndio njia bora zaidi ambayo Mungu hutumia kuwafanya watu kamili; usafishaji na majaribio makali pekee ndiyo yanaweza kusababisha kuonekana upendo wa kweli kwa Mungu ndani ya mioyo ya watu. Bila taabu, watu hukosa upendo wa kweli kwa Mungu; ikiwa hawajaribiwi ndani, na hawapitii usafishaji kwa kweli, basi mioyo yao daima itakuwa ikielea kwa nje. Baada ya kusafishwa hadi kiwango fulani, utayaona mapungufu na matatizo yako mwenyewe, utaona kiasi ambacho unakosa na kwamba huwezi kuzishinda zile shida nyingi unazokabiliwa nazo, na utaona jinsi kutotii kwako kulivyo kukubwa. Ni katika majaribu pekee ndipo watu wataweza kujua kwa kweli hali zao halisi, na majaribu huwafanya watu waweze kufanywa kamili vyema.

Umetoholewa kutoka katika “Ni kwa Kupitia Usafishaji tu Ndiyo Mwanadamu Anaweza Kuwa na Upendo wa Kweli” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 678 Ni Kupitia Taabu na Usafishaji tu Ndiyo Unaweza Kukamilishwa na Mungu

Inayofuata: 680 Upendo wa Mungu Unakuwa Safi Kupitia tu Mateso ya Usafishaji

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp