963 Kutafakari Kujihusu Kwa Njia Hii Ni Muhimu

1 Umuhimu wa kujitafakari na kujijua ni huu: Kadiri unavyozidi kuhisi kuwa katika sehemu fulani umefanya vizuri au umefanya jambo linalofaa, na kadiri unavyofikiri kuwa unaweza kuyaridhisha mapenzi ya Mungu au unastahili kujivunia katika sehemu fulani, basi ndivyo inavyofaa zaidi kwako kujijua katika sehemu hizo na inavyofaa zaidi kwako kuzichunguza zaidi ili kuona ni uchafu gani uko ndani yako, pamoja na mambo gani ndani yako hayawezi kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Hebu tumchukue Paulo kama mfano. Paulo alikuwa mwenye maarifa mno, na alivumilia mengi katika kazi yake ya kuhubiri. Watu wengi walimpenda mno. Kama matokeo, baada ya kumaliza kazi nyingi, alidhani kungekuwa na taji lililowekwa kando kwa ajili yake. Hili lilimfanya atembee zaidi na zaidi kwenye njia isiyo sahihi, hadi mwishowe akaadhibiwa na Mungu.

2 Paulo hakuwa amelenga kutafuta ukweli katika maneno ya Bwana Yesu; alikuwa tu ameamini mawazo na fikira zake mwenyewe. Alikuwa amedhani kwamba almradi afanye mambo machache mazuri na kuonyesha tabia nzuri, angesifiwa na kutuzwa na Mungu. Mwishowe, mawazo na fikira zake zilipofusha roho yake na kufunika hali yake ya kweli. Hadithi hii kumhusu Paulo inatumika kama onyo kwa kila mtu amwaminiye Mungu, ambalo ni kwamba wakati wowote tunapohisi kuwa tumefanya vizuri zaidi, au kuamini kwamba tuna vipawa zaidi katika mambo fulani, au kufikiria kwamba hatuhitaji kubadilika au kushughulikiwa katika jambo fulani, tunapaswa kujitahidi kutafakari na kujijua wenyewe zaidi katika suala hilo; jambo hili ni muhimu. Hii ni kwa sababu bila shaka hujafichua, kutilia maanani au kuchanganua vipengele kujihusu ambavyo mnanafikiri mmefanya vyema, ili kuona kama kweli vina chochote kinachompinga Mungu au la.

3 Kila tendo lako, kila ufanyacho, mwelekeo unaotumia kukifanya, na yale ambayo malengo yako yaliyo, bila shaka, tayari yamedhamiriwa na mawazo na maoni yako. Watu wengine wamejificha vizuri sana, na si dhahiri kwamba wanampinga Mungu kwa njia yoyote. Wao hata hawasemi kuhusu upinzani wowote kwa Mungu. Hata hiyo, mambo ambayo yamekita mizizi akilini mwa mwanadamu yanachukiwa kabisa na Mungu. Hili ndilo Mungu anataka kulifichua na ambalo tunapaswa kulielewa. Ni kwa sababu hii ndiyo Mungu anasema kwamba kadiri unavyozidi kuhisi kwamba unafanya vizuri katika mawanda fulani, ndivyo inavyostahili zaidi wewe ujijue kuhusiana na suala hilo, na kwa hiyo, ndivyo unavyopaswa kuzidi kutafuta ukweli. Ni wakati huo pekee ndiyo unaweza kutakaswa na kukamilishwa na Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Ni kwa Kujua Maoni Yako Yaliyopotoka Tu Ndipo Unapoweza Kujijua Mwenyewe” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Iliyotangulia: 962 Jinsi ya Kuelewa Asili ya Binadamu

Inayofuata: 964 Jielewe Kulingana na Maneno ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

47 Furaha Katika Nchi ya Kanaani

1 Kurudi nyumbani kwa Mungu, nahisi furaha na msisimko. Nina bahati kuona hatimaye Mwenyezi Mungu wa vitendo. Maneno Yake huwaongoza watu...

273 Upendo Safi Bila Dosari

1 Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki