833 Mahitaji Ambayo Mtu Lazima Afikie ili Kukamilishwa

1 Kama kweli uko tayari kukamilishwa na Mungu, basi utakuwa na ujasiri kuweka kando mwili wako, na utaweza kutekeleza maneno ya Mungu na kutokuwa mtu anayekaa tu ama mnyonge. Utaweza kutii yote yatokayo kwa Mungu, na vitendo vyako vyote, viwe vimefanywa hadharani au faraghani, vitastahiki kwa Mungu. Kama wewe ni mtu mwaminifu, na unatenda ukweli katika mambo yote, basi utakamilishwa. Wale wanadamu wadanganyifu wanaotenda njia moja mbele ya wengine na nyingine nyuma yao hawako tayari kukamilishwa. Wote ni wana wa maangamizo na uharibifu; wao si wa Mungu lakini ni wa Shetani. Hao si aina ya wanadamu waliochaguliwa na Mungu! Ukikubali tu hukumu na kuadibu kwa Mungu, na kuweka umuhimu katika mabadiliko ya tabia yako ndipo utafika kwenye njia ya kukamilishwa.

2 Ikiwa kweli uko tayari kukamilishwa na Mungu na kufanya mapenzi ya Mungu, basi unapaswa kutii kazi yote ya Mungu na kutotoa neno lolote la kulalamika, wala hupaswi kutathmini ama kuhukumu kazi ya Mungu utakavyo. Haya ni masharti ya msingi kabisa ya kukamilishwa na Mungu. Mahitaji ya lazima kwa wale wanaotaka kukamilishwa na Mungu ni haya: fanya mambo yote kwa moyo unaompenda Mungu. Inamaanisha kwamba vitendo na tabia yako yote inaweza kuletwa mbele ya Mungu. Kwa sababu una nia sawa, iwapo vitendo vyako ni sawa ama vibaya, huogopi vikionyeshwa kwa Mungu ama kwa ndugu zako; unathubutu kuapa mbele ya Mungu. Lazime uonyeshe kila nia, fikra, na wazo lako mbele ya Mungu ili ayachunguze; ukitenda na kuingia kwa njia hii, basi maendeleo katika maisha yako yatakuwa mepesi.

Umetoholewa kutoka katika “Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 832 Mungu Amedhamiria Kukamilisha Kundi Hili la Watu

Inayofuata: 834 Mungu Huwakamilisha Wale Wanaompenda kwa Dhati

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp