551 Azimio Linalohitajika ili Kufuatilia Ukweli
Je, wengi wenu sasa wana azimio la kuelewa ukweli, kupata ukweli na kukamilishwa mwishowe?
1 Lazima ufikie hatua ambapo azimio lako halibadiliki bila kujali ni mazingira gani unayoyakabili; huku tu ndiko kuwa mwaminifu, na huo ndio upendo halisi wa ukweli na shauku halisi ya kuwa aina hii ya mtu. Itakuwa bure kujikunyata wakati hoja fulani ndogo au shida inapotokea, au kuwa hasi, kusononeka na kuacha azimio lako mwenyewe wakati unapokabiliwa na shida ndogo. Unahitaji kuwa na nguvu ya mtu anayechagua kuhatarisha maisha yake, na kusema, “Bila kujali kinachotokea, hata kama ni lazima nife sitaacha azimio langu au kuachana na lengo hili.” Halafu hakutakuwa na shida ambayo inaweza kukuzuia, na Mungu atakufanyia jambo hili.
2 Lazima uwe na mtazamo wa aina hii na ufahamu jambo linapotokea, na kusema, “Bila kujali kinachofanyika, yote ni sehemu ya kufanikisha lengo langu, na ni shughuli ya Mungu. Kuna udhaifu ndani yangu, lakini mimi si hasi. Ninamshukuru Mungu kwa upendo Anaonipa na kwa kunipangia aina hii ya mazingira. Lazima nisiache matamanio na azimio langu. Kusalimu amri kwangu kungekuwa sawa na kufanya masikilizano na Shetani, na ni sawa na kujiangamiza. Kusalimu amri juu ya shauku na azimio langu kutakuwa sawa na kumsaliti Mungu.” Hii ni aina ya moyo ambao ni lazima uwe nao. Bila kujali wengine wanavyosema au jinsi walivyo, na bila kujali jinsi Mungu anavyokutendea, azimio lako halipaswi kubadilika.
Umetoholewa kutoka katika “Wale Ambao Hawawezi Kuishi Mbele Ya Mungu Daima Ni Wasioamini” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo