165 Amua Kuwa Mtu Mwaminifu

1 Awali, imani yangu katika Bwana ilikuwa kutafuta tu kuelewa nadharia ya kina ya kibiblia. Sikutilia maanani kutenda au kuingia katika matakwa ya Bwana kwamba tuwe watu waaminifu. Nilifanya vitu vilivyomdanganya na kumwasi Mungu, lakini sikuwa na hisia na kutojali. Maombi na sifa zangu za mara kwa mara zilikuwa za kutafuta baraka tu. Niliapa kumpenda Mungu, lakini majaribu yalipotokea nilielewa vibaya na kulalamika. Bidii yangu kwa Bwana ilikuwa tu kwa ajili ya kuvikwa taji na kuzawadiwa. Nilionekana mnyenyekevu na mvumilivu, lakini moyo wangu ulijaa kiburi na udanganyifu. Nilielewa maarifa mengi ya biblia na bado nilikuwa nimefungwa dhambini. Nilifuata njia ya Mafarisayo na nilitamani sana kunyakuliwa kwenda katika ufalme wa mbinguni.

2 Ni leo tu, nipitiapo hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, ndipo nimegutushwa na makosa yangu. Nimeona waziwazi uovu na udanganyifu wangu, kwamba sina mfano wa binadamu. Nilijali tu kuhusu nadharia lakini sijatenda ukweli, nimeenenda katika njia yangu mwenyewe. Hukumu na utakaso wa Mungu hunifanya niishi kwa kudhihirisha mfano wa mtu mwaminifu. Kila moja ya maneno ya Mungu ni ukweli na hata zaidi ni msingi wangu wa jinsi ya kuwa mwanadamu. Kujistahi kulingana na ukweli ni maisha ya heshima, roho yangu iko salama, ina amani. Kiini cha Mungu ni kiaminifu, Anawapenda watu waaminifu na kuwachukia wadanganyifu. Ni watu waaminifu pekee wanaopenda ukweli na ndio watakaobarikiwa zaidi na Mungu. Watu waaminifu wanampenda na kumtii Mungu, ni watu waaminifu pekee wanaoweza kuingia katika ufalme wa mbinguni.

Iliyotangulia: 164 Kupitia Shida, Upendo Wangu kwa Mungu Unaimarishwa

Inayofuata: 166 Tuweze Kujua Uzuri wa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp