832 Mungu Amedhamiria Kukamilisha Kundi Hili la Watu

1 Ni wachache sana miongoni mwa wanadamu wanaouelewa moyo wa Mungu kwa sababu tabia za watu ni duni sana na hisia zao za kiroho zimepoa sana, na kwa sababu hawaoni wala kutilia maanani kile ambacho Mungu anafanya. Hivyo Mungu Anaendelea kuwa na hofu juu ya mwanadamu, kana kwamba asili ya tabia ya wanyama ndani ya mwanadamu inaweza kuonekana muda wowote. Hii inaonyesha zaidi kwamba kuja kwa Mungu duniani kunaambatana na majaribu makubwa. Lakini kwa ajili ya kukamilisha kundi la watu, Mungu, Akiwa na utukufu, Alimwambia mwanadamu juu ya kila kusudi lake, bila kuficha kitu.

2 Ameamua kwa dhati kukamilisha kundi hili la watu. Kwa hiyo, ije shida yoyote au jaribu, Anatazama mbali na kuyapuuzia yote. Anafanya kazi yake kimyakimya tu, Akiamini kwamba siku moja ambapo Mungu Atapata utukufu, mwanadamu atamjua Mungu, na kuamini kwamba mwanadamu atakapokuwa amekamilishwa na Mungu, atakuwa ameuelewa moyo wa Mungu kikamilifu. Sasa hivi kunaweza kuwepo watu wanaomjaribu Mungu au kumwelewa vibaya Mungu au kumlaumu Mungu; Mungu wala hayazingatii haya moyoni. Mungu atakapoingia katika utukufu, watu wote wataelewa kwamba kila kitu ambacho Mungu Anafanya ni kwa ajili ya mema ya binadamu, na watu wote wataelewa kwamba kila kitu ambacho Mungu Anafanya ni kwa sababu binadamu aweze kuishi vizuri.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi na Kuingia (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 831 Amini Kwamba Mungu Hakika Atamfanya Mwanadamu Mkamilifu

Inayofuata: 833 Mahitaji Ambayo Mtu Lazima Afikie ili Kukamilishwa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp