804 Matokeo Yanayofanikishwa na Kumjua Mungu

1 Mpaka siku moja, utahisi kuwa Muumba sio fumbo tena, kwamba Muumba hajawahi kufichwa kutoka kwako, kwamba Muumba hajawahi kuificha sura Yake kutoka kwako, kwamba Muumba hayuko mbali na wewe hata kidogo, kwamba Muumba siye yule unayemtamania katika mawazo yako lakini kwamba huwezi kumfikia na hisia zako, kwamba Anasimama kwa kweli kama mlinzi kulia na kushoto kwako, Akiruzuku maisha yako, na kudhibiti majaliwa yako. Hayuko katika upeo wa mbali, wala hajajificha juu mawinguni. Yuko kando yako, akiwa na mamlaka juu ya kila kitu chako, Yeye ni kila kitu ulicho nacho, na Yeye ni kitu pekee ulicho nacho.

2 Mungu kama huyo Anakukubali umpende kutoka moyoni, umshikilie, umweke karibu, umtamani, uhofu kumpoteza, na kutotaka kumkataa tena, kutomtii tena, ama kumwepuka tena ama kumweka mbali. Kile unachotaka ni kumjali tu, kumtii, kulipia kila kitu Anachokupa, na kujisalimisha katika himaya Yake. Hukatai tena kuongozwa, kupewa, kuangaliwa, na kuwekwa na Yeye, hukatai tena Anachoamuru na kukitawaza kwako. Unachotaka tu ni kumfuata, kutembea kando Yake katika kushoto ama kulia Kwake, kile utakacho ni kumkubali kama maisha yako ya pekee, kumkubali kama Bwana wako mmoja na wa pekee, Mungu wako mmoja na wa pekee.

Umetoholewa kutoka katika “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 803 Ni kwa Kumjua Mungu tu Ndiyo Unaweza Kumwabudu kwa Kweli

Inayofuata: 805 Ni Wale tu Wanaomjua Mungu Ndio Wanaweza Kumshuhudia

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp