Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Wale Wanaomcha Mungu Humtukuza Mungu Katika Vitu Vyote

1 Ingawaje Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu au kusikia maneno ya Mungu kwa masikio yake mwenyewe, Mungu alikuwa na nafasi katika moyo wa Ayubu. Na mwelekeo wa Ayubu kwa Mungu ulikuwa upi? Ulikuwa, kama ulivyorejelewa awali, “jina la Yehova libarikiwe.” Baraka yake kwa jina la Mungu haikuwa ya masharti, pasipo kujali muktadha, na bila ya sababu. Tunaona kwamba Ayubu alikuwa ameukabidhi moyo wake kwa Mungu, na kuuruhusu kudhibitiwa na Mungu; kila kitu alichofikiria, kila kitu alichoamua, na kila kitu alichopangilia katika moyo wake kilikuwa wazi kwa Mungu na wala moyo wake haukuwa umefungwa kuzuia Mungu. Moyo wake haukumpinga Mungu, na hakuwahi kuuliza Mungu kumfanyia chochote au kumpa chochote yeye, na wala hakuwa na matamanio yasiyo ya kawaida ambayo angepata chochote kutoka kwa kumwabudu Mungu.

2 Ayubu hakuzungumzia biashara na Mungu, na wala hakutoa ombi lolote au madai yoyote kwa Mungu. Hali yake ya kusifia jina la Mungu ilikuwa kwa sababu ya nguvu kuu na mamlaka ya Mungu katika kutawala mambo yote, na haikutegemea kama alipata baraka au alipigwa na janga. Aliamini kwamba haijalishi kama Mungu anawabariki watu au analeta janga kwao, mamlaka na nguvu vyote havitabadilika, na hivyo, haikujalisha hali za mtu, jina la Mungu linafaa kusifiwa. Kwamba binadamu amebarikiwa na Mungu ni kwa sababu ya ukuu wa Mungu, na wakati janga lilipompata binadamu, hivyo, pia ni kwa sababu ya ukuu wa Mungu. Nguvu na mamlaka ya Mungu vyote vinatawala na kupangilia kila kitu cha binadamu; matukio yasiyo ya kawaida kuhusu utajiri wa binadamu ni maonyesho ya nguvu na mamlaka ya Mungu.

3 Na licha ya maoni yake mtu, jina la Mungu linafaa kusifiwa. Haya ndiyo ambayo Ayubu alipitia na kuishia kujua katika miaka ya maisha yake. Fikira na matendo yote ya Ayubu vyote vilifikia masikio ya Mungu na vikawasili mbele ya Mungu, na vikaonekana kuwa muhimu na Mungu. Mungu aliyapenda sana maarifa haya ya Ayubu na akathamini sana Ayubu kwa kuwa na moyo kama huo. Moyo huu ulisubiria amri ya Mungu siku zote, na pahali pote, na haijalishi ni muda au mahali gani palipokaribisha chochote kile kilichomsibu. Ayubu hakutoa mahitaji yoyote kwa Mungu. Kile alichohitaji kutoka kwake kilikuwa kusubiria, kukubali, kukabiliana na kutii mipangilio yote iliyotoka kwa Mungu; Ayubu alisadiki hili kuwa wajibu wake, na ndio hasa kile ambacho Mungu Alitaka.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia:Uzuri wa Ufalme

Inayofuata:Ni Wale tu Wanaomcha Mungu Ndio Wanaweza Kumshuhudia Katika Majaribio

Maudhui Yanayohusiana