161 Chanzo cha Mwanadamu Kumpinga na Kutomtii Kristo
1 Uungu wa Kristo ni zaidi ya wanadamu wote, kwa hivyo Yeye Anayo mamlaka ya juu ya viumbe vyote vilivyoumbwa. Mamlaka haya ni uungu Wake, yaani, nafsi na tabia ya Mungu Mwenyewe, ambayo huamua utambulisho Wake. Kwa hiyo, haijalishi jinsi ubinadamu Wake ni wa kawaida ni wazi kuwa Anao utambulisho wa Mungu Mwenyewe; haijalishi upande Anaosimama Akiongea na kwa vyovyote vile Yeye hutii mapenzi ya Mungu, haiwezi kusemwa kwamba Yeye si Mungu Mwenyewe.
2 Wanadamu wajinga na wapumbavu mara nyingi huchukua ubinadamu wa kawaida wa Kristo kama dosari. Haijalishi jinsi Anavyofichua na kuonyesha nafsi ya uungu Wake, mwanadamu bado hawezi kukiri kwamba Yeye ni Kristo. Na zaidi kwamba Kristo Anaonyesha utii Wake na unyenyekevu, ndivyo wanadamu wengi wajinga humchukua Kristo kwa mzaha. Kuna hata wale ambao huelekeza Kwake mtizamo wa kutengwa na dharau, ilhali kuweka wale “wanadamu wakubwa” wa picha ya kujidai juu ya meza na kuwaabudu. Upinzani wa binadamu dhidi ya, na uasi wa Mungu huja kutokana na ukweli kwamba kiini cha Mungu mwenye mwili hutii mapenzi ya Mungu, vile vile kutokana ubinadamu wa kawaida wa Kristo; hapa ndipo kuna chanzo cha upinzani wa binadamu na uasi wake kwa Mungu.
Umetoholewa kutoka katika “Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni” katika Neno Laonekana katika Mwili