267 Shetani Huyadhibiti Mawazo kwa Umaarufu na Mali

1 Kwa hivyo Shetani hutumia umaarufu na faida kudhibiti fikira za mwanadamu hadi anachofikiria tu ni umaarufu na faida. Wanapambana kwa sababu ya umaarufu na faida, wanateseka matatizo kwa sababu ya umaarufu na faida, wanastahimili udhalilishaji kwa sababu ya umaarufu na faida, wanatoa kila kitu walichonacho kwa sababu ya umaarufu na faida, na watafanya maoni au uamuzi wowote kwa ajili ya umaarufu na faida. Kwa njia hii, Shetani humfunga mwanadamu kwa pingu zisizoonekana. Pingu hizi zinabebwa na watu, na hawana nguvu ama ujasiri wa kuzirusha mbali. Kwa hivyo, bila kujua, watu huvumilia pingu hizi na kutembea kwenda mbele kwa ugumu mkubwa. Kwa ajili ya umaarufu huu na faida hii, binadamu humwepuka Mungu na kumsaliti, na wanazidi kuwa waovu zaidi na zaidi. Kwa njia hii, hivyo kizazi kimoja baada ya kingine kinaharibiwa katika umaarufu na faida ya Shetani.

2 Pengine leo bado hamwezi kuona kupitia nia husuda za Shetani kwa sababu mnafikiri hakuna maisha bila umaarufu na faida. Mnafikri kwamba, iwapo watu wataacha umaarufu na faida nyuma, basi hawataweza tena kuona njia mbele, hawataweza tena kuona malengo yao, siku zao za baadaye zawa giza, zilizofifia na za ghamu. Lakini, polepole, nyote siku moja mtatambua kwamba umaarufu na faida ni pingu za ajabu ambazo Shetani hutumia kumfunga mwanadamu. Hadi ile siku utakuja kutambua hili, utapinga kabisa udhibiti wa Shetani na utapinga kabisa pingu anazoleta Shetani kukufunga. Wakati utakapofika wa wewe kutaka kutupilia mbali vitu vyote ambavyo Shetani ameingiza ndani yako, utakuwa basi umejiondoa kwa Shetani na pia utachukia kwa kweli vyote ambavyo Shetani amekuletea. Hapo tu ndipo utakuwa na upendo na shauku ya kweli kwa Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 266 Binadamu Wahitaji Ruzuku ya Mungu ya Uzima

Inayofuata: 268 Jinsi Shetani Atumiavyo Mitindo ya Kijamii Kumpotosha Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp