924 Asili ya Shetani ni Katili na Ovu
1 Shetani hupata umaarufu wake kupitia kwa kuudanganya umma. Mara nyingi hujiweka kama kiongozi na kuchukua wajibu wa kielelezo cha haki. Akisingizia kuwa anasalimisha haki, anaishia kumdhuru binadamu, kudanganya nafsi zao, na kutumia mbinu zote ili kuweza kuteka nyara hisia na fikira za binadamu, kumdanganya na kumchochea. Shabaha yake ni kumfanya binadamu kuidhinisha na kuufuata mwenendo wake wa maovu, kumfanya binadamu kujiunga naye katika kupinga mamlaka na ukuu wa Mungu. Hata hivyo, wakati mtu anapokuwa mwerevu na kutambua njama zake, mipango na sifa zake hizo na hataki kuendelea kudhalilishwa na kudanganywa naye hivyo au kuendelea kuwa mtumwa wa Shetani, au kuadhibiwa na kuangamizwa pamoja na Shetani, Shetani naye hubadilisha sifa zake za awali za utakatifu na kuondoa baraka yake bandia ili kufichua uso wake wa kweli wenye maovu, ubaya, sura mbaya na wa kikatili. Shetani hawezi kupenda jambo lolote isipokuwa kumaliza wale wote wanaokataa kumfuata yeye na wale wanaopinga nguvu zake za giza.
2 Wakati huu Shetani hawezi tena kuvaa sura ya uaminifu, na utulivu; badala yake, sifa zake za kweli za sura mbaya na za kishetani zilizokuwa zimefichwa kwenye mavazi ya kondoo zinafichuliwa. Mara tu njama za Shetani zinapomulikwa, na sifa zake za kweli kufichuliwa, yeye huingia kwenye hisia za hasira kali na kuonyesha ushenzi wake; tamanio lake la kudhuru na kudanganya watu ndipo litazidi zaidi. Hii ni kwa sababu anapandwa na hasira kali kwa kuzindukana kwa binadamu; anataka kuwa na kisasi kingi dhidi ya binadamu kwa maazimio yake ya kutamani kuwa na uhuru na nuru na kutokuwa mateka wa jela yake. Hasira yake kali inanuiwa kutetea maovu yake, na pia ni ufunuo wa kweli wa asili yake ya kishenzi.
Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II” katika Neno Laonekana katika Mwili