539 Ushawishi wa Shetani Hauwezi Kutupiliwa Mbali Bila Kufuatilia Ukweli

1 Wakati Mungu aliumba watu, ilikuwa ili kuwafanya wafurahie utajiri Wake na wampende kwa kweli; katika njia hii, watu wangeishi katika nuru Yake. Leo, wote ambao hawawezi kumpenda Mungu, ambao hawako makini kwa mizigo Yake, ambao hawawezi kutoa mioyo yao kikamilifu kwa Mungu, ambao hawawezi kuchukua moyo wa Mungu kama wao wenyewe, ambao hawawezi kubeba mizigo ya Mungu kama yao wenyewe—nuru ya Mungu haiangazi juu ya watu wowote kama hawa, kwa hivyo, wote wanaishi chini ya ushawishi wa giza. Wako kwenye njia ambayo huenda kinyume kabisa na mapenzi ya Mungu, na yote wanayoyafanya hayana hata chembe ya ukweli. Wanazamia katika matatizo na Shetani na ni wale ambao wanaishi chini ya ushawishi wa giza. Wale wote ambao hawawezi kukubali kazi ya Mungu au wanaokubali kazi ya Mungu lakini hawawezi kukidhi matakwa Yake wanaishi chini ya ushawishi wa giza; wale tu wanaofuatilia ukweli na wana uwezo wa kukidhi matakwa ya Mungu watapokea baraka kutoka Kwake, na ni wao tu wataepuka ushawishi wa giza.

2 Wote ambao humwamini Mungu ilhali hawafuatilii ukweli hawana namna ya kuepuka ushawishi wa shetani. Wale wote ambao hawaishi maisha yao kwa uaminifu, wanaotenda kwa njia moja mbele ya wengine na njia nyingine kwa siri, wanaotoa mwonekano wa unyenyekevu, uvumilivu, na upendo ilhali katika kiini ni wenye kudhuru kwa siri, wana hila, na hawana uaminifu kwa Mungu—watu hawa ni mfano halisi wa wale wanaoishi chini ya ushawishi wa giza. Wao ni wa kizazi cha nyoka. Wale ambao imani yao katika Mungu daima ni kwa ajili ya faida zao wenyewe, ambao ni wa kujidai na wenye maringo, ambao hujigamba, na hulinda hadhi zao wenyewe ni wale wanaompenda Shetani na kuupinga ukweli. Wao wanapinga Mungu na ni wa Shetani kikamilifu. Wale ambao hawako makini kwa mizigo ya Mungu, ambao hawamtumikii Mungu kwa moyo wote, ambao daima wanajali maslahi yao wenyewe na maslahi ya familia zao, ambao hawawezi kuacha kila kitu ili wajitumie kwa ajili ya Mungu, na ambao kamwe hawaishi kulingana na maneno Yake wanaishi nje ya maneno ya Mungu. Watu kama hawa hawawezi kupokea sifa ya Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Epuka Ushawishi wa Giza na Utapatwa na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 538 Mwanadamu Aokolewa Anapotupa Mbali Ushawishi wa Shetani

Inayofuata: 540 Tupilia Mbali Ushawishi wa Giza ili Upatwe na Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp