538 Mwanadamu Aokolewa Anapotupa Mbali Ushawishi wa Shetani

1 Mwili wa mwanadamu ni wa Shetani, umejaa tabia za uasi, ni mchafu kiasi cha kusikitisha, na ni kitu chenye najisi. Watu hutamani raha ya mwili kupita kiasi na kuna maonyesho mengi sana ya mwili; hii ndiyo maana Mungu hudharau mwili wa mwanadamu kwa kiwango fulani. Watu wanapotupa mambo machafu, potovu ya Shetani, wao hupata wokovu wa Mungu. Lakini bado wasipoachana na uchafu na upotovu, basi bado wanamilikiwa na Shetani.

2 Ujanja, udanganyifu, na ukora wa watu yote ni mambo ya Shetani. Wokovu wa Mungu kwako ni ili kukuokoa kutoka katika mambo haya ya Shetani. Kazi ya Mungu haiwezi kuwa na kosa; yote inafanywa ili kuwaokoa watu kutoka gizani. Wakati ambapo umeamini hadi kwa kiwango fulani na unaweza kuachana na upotovu wa mwili, na hufungwi tena pingu na upotovu huu, je, hutakuwa umeokolewa? Wakati ambapo unamilikiwa na Shetani huwezi kumdhihirisha Mungu, wewe ni kitu kichafu, na huwezi kupokea urithi wa Mungu. Mara tu unapotakaswa na kufanywa mkamilifu, utakuwa mtakatifu, utakuwa mtu wa kawaida, na utabarikiwa na Mungu na kuwa mtu anayemfurahisha Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Utendaji (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 537 Kuelewa Ukweli Ukaribiapo Kufa Kumechelewa Sana

Inayofuata: 539 Ushawishi wa Shetani Hauwezi Kutupiliwa Mbali Bila Kufuatilia Ukweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp