547 Mungu Awaokoa Wale Wanaopenda Ukweli

1 Mambo ambayo hufanyika kila siku, yawe ni makubwa ama madogo, yanaweza kutikisa uthabiti wako, kuumiliki moyo wako, kuzuilia uwezo wako wa kufanya jukumu lako, ama kudhibiti kuendelea kwako mbele—vitu hivi vyote vinahitaji kuchukuliwa kwa uzito, lazima vichunguzwe kwa makini ili kuutafuta ukweli, na ni vitu vyote ambavyo vinafanyika katika ulimwengu wa uzoefu. Watu wengine huacha kazi zao wakati kitu kibaya kinawafikia, na wanashindwa kusimama baada ya kila pingamizi. Watu hawa wote ni wapumbavu ambao hawapendi ukweli, na watakosa kupata ukweli hata wakiishi maisha yao yote kwa imani. Watu wapumbavu kama hao watawezaje kufuata hadi mwisho?

2 Watu werevu na wale ambao kwa kweli wana ubora wa ndani na wanaelewa masuala ya kiroho ni watafutaji wa ukweli, na mara nane kwa kumi pengine wanaweza kupata ufunuo kiasi, funzo, kupata nuru na maendeleo. Kitu kama hicho kinapofanyika kwa mpumbavu asiyeelewa masuala ya kiroho, mara kumi, anajikwaa mara kumi, lakini bado hazinduki, wala hatafuti ukweli kutafuta kiini cha shida. Bila kujali jinsi mtu wa aina hii huenda akasikiza mahubiri, hatawahi kuelewa ukweli—ameshindwa tu. Kila wakati anapojikwaa anahitaji mtu mwingine kumsaidia kusimama tena, kumbembeleza. Watu hawa ni bure na Mungu hawaokoi.

3 Wokovu wa Mungu kwa binadamu ni wokovu kwa wale wanaopenda ukweli. Ni wokovu kwa wale wenye dhamira na azimio, wale wanaotamani ukweli na haki. Kusema mtu ana azimio kunamaanisha kuwa anataka sana haki, uzuri na ukweli, na kuwa ana dhamiri. Mungu hufanya kazi ndani ya watu hawa ili waweze kuelewa na kupata ukweli, ili upotovu wao uweze kutakaswa na tabia ya maisha yao iweze kubadilishwa. Ikiwa ndani yako hakuna upendo wa ukweli ama hamu ya haki na mwanga, basi hakuna njia ya kuokolewa.

Umetoholewa kutoka katika “Watu Waliochanganyikiwa Hawawezi Kuokolewa” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Iliyotangulia: 546 Mungu Huwapenda Wale Wanaofuatilia Ukweli

Inayofuata: 548 Mungu Awapenda Wale Walio na Azimio

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

125 Nimeuona Upendo wa Mungu

1Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda.Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi!Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako,...

137 Nitampenda Mungu Milele

1Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako.Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku.Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu na...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki