590 Lazima Utafute Mapenzi ya Mungu Katika Vitu Vyote

1 Punde tu watu wanapokuwa na haraka wakati wakiutimiza wajibu wao, hawajui jinsi ya kuuzoea; punde tu wanaposhughulika na mambo, hali yao ya kiroho inakuwa na matatizo; hawawezi kudumisha hali yao ya kawaida. Inawezekanaje kuwa hivi? Unapoombwa kufanya kazi kidogo, haufuati ukawaida, unakosa mipaka, husogei karibu na Mungu na unajitenga mbali na Mungu. Hili linadhibitisha kwamba watu hawajui jinsi ya kuwa na uzoefu. Haidhuru nini ufanyalo, unapaswa kwanza kuelewa kwa nini unalifanya, nia inayokupeleka kulifanya jambo hili ni gani, umuhumu ni gani katika wewe kulifanya, asili ya jambo hilo ni ipi, na iwapo ufanyalo ni jambo chanya au jambo hasi. Lazima uwe na ufahamu dhahiri kuhusu masuala haya yote; hii inahitajika sana kuweza kutenda kulingana na kanuni. Ikiwa unafanya kitu kutimiza wajibu wako, basi unapaswa kutafakari: Nitalifanyaje hili? Nitatimizaje wajibu wangu vyema ili nisiwe nafanya kwa uzembe tu? Unapaswa kusogea karibu na Mungu katika jambo hili.

2 Kusogea karibu na Mungu kunamaanisha kutafuta ukweli katika jambo hili, kutafuta njia ya kutenda, kutafuta mapenzi ya Mungu, kutafuta jinsi ya kumridhisha Mungu. Haihusu kufanya taratibu za kidini au tendo lionekanalo kwa nje. Inafanywa kwa kusudi la kutenda kulingana na kweli baada ya kutafuta mapenzi ya Mungu. Unapotimiza wajibu wako au kushughulikia kitu, unapaswa daima kufikiri: Ninapaswaje kutimiza wajibu huu? Mapenzi ya Mungu ni yapi? Ni ili wewe usogee karibu na Mungu kupitia unachofanya, na, kwa hufanya hivyo, unazitafuta kanuni na ukweli wa matendo yako pamoja na mapenzi ya Mungu, na usipotee kutoka kwa Mungu katika chochote utendacho. Mtu wa aina hii tu ndiye anayemwamini Mungu kwa kweli. Siku hizi, kila wakati ambapo watu wanakumbana na mambo, wanaendelea tu kwa ukaidi, na kutenda kulingana na nia zao binafsi. Watu wa aina hii hawana Mungu ndani yao, ni wabinafsi tu moyoni mwao na hawawezi tu kuuweka ukweli katika matendo katika kitu chochote afanyacho.

3 Kutotenda kulingana na ukweli kunamaanisha kufanya vitu kulingana na mapenzi yao wenyewe, na kufanya vitu kulingana na mapenzi yao wenyewe kunamaanisha kumwacha Mungu; yaani, Mungu hayupo ndani ya ndani ya mioyo yao. Mawazo ya binadamu kwa kawaida yanaonekana mazuri na sahihi kwa watu, na yanaonekana kana kwamba hayawezi kukiukaukweli kwa kiasi kikubwa sana. Watu huhisi kwamba kufanya mambo kwa jinsi hii kutakuwa kuweka ukweli katika matendo; wanahisi kwamba kufanya mambo kwa jinsi hiyo kutakuwa kumtii Mungu. Hakika, hawamtafuti Mungu kwa kweli au kumwomba Mungu kulihusu, na hawajitahidi kulifanya vizuri kulingana na mahitaji ya Mungu, ili kuridhisha mapenzi Yake. Hawamiliki hali hii ya kweli, wala hawana hamu kama hiyo. Hili ndilo kosa kubwa zaidi ambalo watu hufanya katika kutenda kwao. Unamwamini Mungu, lakini humweki Mungu moyoni mwako. Hii sio dhambi vipi? Je, hujidanganyi mwenyewe? Ni aina gani za athari ambazo unaweza kuvuna ukiendelea kuamini jinsi hiyo? Isitoshe, umuhimu wa imani unaweza kuonyeshwa vipi?

Umetoholewa kutoka katika “Kutafuta Mapenzi ya Mungu ni Kwa Ajili ya Kutenda Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 589 Mungu Aliwaandalia Wanadamu Kila Kitu Kitambo

Inayofuata: 591 Utoe Uaminifu Wako kwa Ajili ya Nyumba ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp