842 Unapaswa Kutafuta Kukamilishwa na Mungu Katika Vitu Vyote

1 Kwa sasa, kile ambacho mnafaa kutafuta kimsingi ni kukamilishwa na Mungu katika mambo yote, na kukamilishwa na Mungu kupitia kwa watu wote, mambo yote na vitu vyote ambavyo mnakumbwa navyo, ili mambo zaidi ya kile Mungu Alicho yatashirikishwa ndani yenu. Lazima kwanza mpokee urithi wa Mungu ulimwenguni kabla ya kustahili kurithi baraka nyingi na kubwa zaidi kutoka kwa Mungu. Mambo yote haya ndiyo ambayo mnafaa kutafuta na ambayo kwanza mnafaa kuelewa. Zaidi unavyotafuta kukamilishwa na Mungu katika mambo yote, ndivyo utakavyoweza kuona mkono wa Mungu zaidi katika mambo yote, na hivyo kutafuta kwa bidii kuingia katika hali ya neno la Mungu na uhalisia wa neno Lake kupitia mitazamo tofauti na katika mambo tofauti. Huwezi kutosheka na hali hasi kama kutotenda dhambi tu, au kutokuwa na dhana, kutokuwa na filosofia ya kuishi, na kutokuwa na hiari ya binadamu.

2 Mungu humkamilisha mwanadamu kwa njia tofauti, na inawezekana katika mambo yote kwako kukamilishwa hatimaye. Huwezi tu kukamilishwa kwa kuzingatia mambo halisi, lakini pia mambo hasi, na hivyo kuboresha kile unachopata. Kila siku kunazo fursa za kukamilishwa na muda wa kupatwa na Mungu. Baada ya kipindi cha kupitia mambo kama haya, utabadilika pakubwa. Utaweza sasa kimaumbile kufaidi utambuzi katika mambo mengi ambayo hukuyaelewa awali; bila ya kuhitaji wengine kukufunza, bila kujua, utaweza kufahamishwa na Mungu, ili uweze kuwa na fahamisho katika mambo yote na mambo yote utakayopitia yatakuwa mengi. Mungu atakuongoza wewe ili usije ukapotoka kwa vyovyote vile. Kisha utawekwa wazi kwenye njia ya kufanywa kuwa mtimilifu na Yeye.

Umetoholewa kutoka katika “Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 841 Njia ya Kukamilishwa na Mungu

Inayofuata: 843 Wewe ni Mtu Anayetafuta Kukamilishwa na Mungu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp