525 Tafuta Kuwa Yule Anayemwabudu Mungu kwa Kweli

1 Je, kutafuta kuwa mtu anayemwabudu Mungu kwa dhati ni mtazamo tunaopaswa kuwa nao? Kutompinga Mungu tena, kutomkera tena, kutomfanya Mungu kukerwa nasi na kukasirika nasi daima, kuufariji moyo wa Mungu, kuwa mtu anayemwabudu Mungu kwa kweli kama Ibrahimu—je, hii ni mitazamo juu ya maisha ambayo tunapaswa kuwa nayo?Ukiwa na aina hii ya mtazamo juu ya maisha na aina hii ya kufikiri iliyokita mizizi akilini mwako, ufuatiliaji wako unapokuwa ukielekea upande huu, je, si majaribu ya utajiri wa kidunia, hadhi na sifa yatakuwa ndogo zaidi? Je, si mvuto utakuwa mdogo zaidi?

2 Wakati kazi yako ya bidii, mazoezi, na uzoefu vinaelekea mtazamo huu, bila kutambua maneno ya Mungu yatakuwa wito ndani mwako, msingi wa kuishi kwako, maneno Yake yatakuwa maisha yako, na yatakuwa njia yako katika maisha ndani mwako. Wakati huo, mambo yote ya ulimwengu huu hayatakuwa muhimu tena kwako. Kwa hivyo, mtazamo kuhusu maisha ambao mtu anapaswa kuwa nao ni kufuatilia kuwa mtu aliye na ukweli na ubinadamu, mtu aliye na dhamiri na mantiki na humwabudu Mungu—yaani, kuwa mtu wa kweli—huku ndiko kufuatilia kunakostahili kabisa.

Umetoholewa kutoka katika “Nini Maana ya Mabadiliko Katika Tabia na Njia Kuelekea Mabadiliko Katika Tabia” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 524 Neno la Mungu Kweli Limekuwa Maisha Yako?

Inayofuata: 526 Pamoja Na Ukweli Kuna Nguvu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp