947 Tafuta Ukweli Katika Kila Kitu

1 Haidhuru unachokifanya, haidhuru jambo ni kubwa kiasi gani, na bila kujali kama unatimiza wajibu wako katika familia ya Mungu, au kama ni jambo lako la kibinafsi, lazima ufikirie kama jambo hili linalingana na mapenzi ya Mungu, kama jambo hili ni kitu ambacho mtu ambaye ana ubinadamu anapaswa kufanya, na kama kile unachokifanya kitamfanya Mungu awe na furaha. Unahitaji kufikiria kuhusu vitu hivi. Utakapofanya hivi, basi wewe ni mtu anayetafuta ukweli na mtu ambaye anamwamini Mungu kwa kweli. Ukishughulikia kwa moyo wote kila jambo na kila kweli kwa jinsi hii, basi utaweza kubadilisha tabia yako.

2 Watu wengine wanafikiri ya kwamba wanafanya kitu cha kibinafsi, kwa hivyo wanaupuuza ukweli, wakifikiria: Hili ni jambo la faragha, na nitalifanya nitakavyo. Wanalifanya kwa njia yoyote ile inayowafanya wawe na furaha, na kwa njia yoyote ile iliyo na faida kwao; hawafikirii hata kidogo zaidi jinsi itakavyoathiri familia ya Mungu na hawafikirii kama inalingana na mpango wa watakatifu. Hatimaye, wanapomaliza jambo hili, wana giza ndani yao na wana wasiwasi; Je hii sio adhabu iwafaayo? Ukifanya vitu ambavyo havijaidhinishwa na Mungu basi umemkosea Mungu. Ikiwa watu hawaupendi ukweli, na mara nyingi wanafanya vitu kulingana na mapenzi yao, basi watamkosea Mungu mara kwa mara. Aina hii ya mtu kwa kawaida hapewi idhini na Mungu kwa yale ayatendayo na ikiwa hatageuka, basi hatakuwa mbali na adhabu.

Umetoholewa kutoka katika “Kutafuta Mapenzi ya Mungu ni Kwa Ajili ya Kutenda Ukweli” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Iliyotangulia: 946 Ni Wale Tu Wamchao Mungu Ambao Huishi Kwa Heshima

Inayofuata: 949 Kufanya Kazi kwa Uzembe Si Kutekeleza Wajibu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

132 Mradi tu Usimwache Mungu

Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki