517 Tafuta Ukweli katika Vitu Vyote ili Kuendelea Mbele

1 Mungu akipanga mazingira, watu, vitu, na mambo fulani kwa ajili yako, Akikupogoa na kukushughulikia na ukijifunza kutokana na hili, ikiwa umejifunza kuja mbele za Mungu kutafuta ukweli, na, bila kujua, umetiwa nuru na kuangaziwa na kupata ukweli, ikiwa umepitia mabadiliko katika mazingira haya, umepata thawabu, na kupiga hatua, ukianza kuwa na ufahamu mdogo kuhusu mapenzi ya Mungu na kuacha kulalamika, basi yote haya yatamaanisha kuwa umesimama imara katikati ya majaribio ya mazingira haya, na umestahimili jaribio. Kwa hiyo, utakuwa umeshinda majaribu haya.

2 Wale ambao huhimili jaribio wana moyo wa kweli, wanaweza kuvumilia mateso ya aina hii na ndani yao kabisa, wanapenda ukweli na wanataka ukweli. Ikiwa Mungu ana makadirio ya aina hii kutoka kwako, basi wewe ni mtu mwenye kimo, na una uzima. Na uzima huu hupatikanaje? Hutolewa na Mungu; ni Mungu kuja Yeye binafsi kukuletea bakuli la chakula na kulileta hadi kinywani mwako; basi, mara unapokula, unahisi kutosheka na unaweza kusimama imara. Hii ndiyo jinsi ya kuwa mtiifu kwa kila kitu kutoka kwa Mungu.

3 Lazima uwe na hali ya akili ya aina hii na mtazamo wa aina hii, na lazima ujifunze kutafuta ukweli. Ni sharti usitafute kila mara sababu za nje au kuwalaumu wengine kwa ajili ya shida zako, na lazima uelewe nia ya Mungu. Kutoka nje, watu wengine wanaweza kuonekana kuwa na maoni juu yako au upendeleo dhidi yako, lakini hupaswi kuona mambo kwa njia hiyo. Ukitazama vitu kwa mtazamo usio sahihi, jambo la pekee utakalofanya ni kutoa sababu ili kuwashawishi wengine, na hutaweza kupata chochote. Unapaswa kuelewa mambo bila upendeleo na kwa usawa; kwa njia hiyo, utatafuta ukweli na kuelewa nia ya Mungu. Mara maoni na hali yako ya akili vitakaporekebishwa, utaweza kupata ukweli.

Umetoholewa kutoka katika “Ili Kupata Ukweli, Lazima Ujifunze Kutoka kwa Watu, Mambo, na Vitu Vinavyokuzunguka” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 516 Kubali Neno la Mungu ili Uwe na Uzoefu wa Kina

Inayofuata: 518 Kuelewa Ukweli Si Jambo Rahisi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp