709 Tafuta Ukweli ili Upate Mabadiliko Katika Tabia

1 Kwa kufuatilia ukweli tu ndipo mtu anaweza kutimiza mabadiliko katika tabia: Hili ni jambo ambalo watu wanafaa kufahamu na kulielewa vizuri kabisa. Usipokuwa na ufahamu wa kutosha wa ukweli, utateleza kwa urahisi na kupotoka. Kama kwa kweli una ukweli ndani yako, njia unayotembea kiasili itakuwa njia sahihi. Bila ukweli, ni rahisi kufanya uovu na hutakuwa na budi kuufanya. Kwa mfano, kama kiburi na majivuno, vingekuwa ndani yako, ungeona kwamba haiwezekani kuepuka kumwasi Mungu; ungehisi kulazimishwa kumwasi. Hutafanya hivyo kimakusudi; utafanya hivyo chini ya utawala wa asili yako ya kiburi na majivuno. Kiburi na majivuno yako vitakufanya umdharau Mungu na kumwona kuwa asiye na maana; vitakufanya ujiinue, vitakufanya kujiweka kila wakati kwenye maonyesho, na mwishowe vitakufanya ukae katika nafasi ya Mungu na kujitolea ushuhuda mwenyewe. Mwishowe utayabadilisha mawazo yako mwenyewe, fikira zako mwenyewe na dhana zako yawe ukweli wa kuabudiwa. Tazama ni kiasi gani cha uovu kinafanywa na watu chini ya utawala wa asili yao ya kiburi na majivuno!

2 Kutatua matendo yao maovu, lazima kwanza watatue matatizo ya asili yao. Bila mabadiliko katika tabia, haitawezekana kuleta suluhu ya kimsingi kwa shida hii. Unapokuwa na uelewa fulani wa Mungu, unapoweza kuona upotovu wako mwenyewe na kutambua uhafifu na ubaya wa kiburi na majivuno, basi utahisi chuki, kughadhabishwa na kutatizwa. Utaweza kufanya mambo kwa ufahamu kumridhisha Mungu na kwa kufanya hivi, utahisi utulivu. Utaweza kwa ufahamu kutoa ushuhuda kwa Mungu na kwa kufanya hivi, utahisi raha. Kwa ufahamu utajifichua mwenyewe, huku ukifunua ubaya wako, na kwa kufanya hivi, utahisi vizuri ndani yako na kujihisi kuwa katika hali iliyoboreka ya akili. Hivyo basi, hatua ya kwanza ya kutafuta mabadiliko katika tabia yako ni kutafuta kuyaelewa maneno ya Mungu na kuingia katika ukweli. Ni kwa kuuelewa tu ukweli ndio unaweza kufikia utambuzi; ni kwa kuwa na utambuzi tu ndio unaweza kuelewa mambo kabisa; ni kwa kuelewa mambo tu kwa wazi ndio unaweza kuutelekeza mwili na, hatua kwa hatua, kuwa kwa njia sahihi ukiwa na imani kwa Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Ni Kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 708 Mchakato wa Badiliko Katika Tabia

Inayofuata: 710 Tabia Yako Inaweza Kubadilika Tu kwa Kutii Kazi ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp